TAARIFA KWA UMMA
1.0
UTANGULIZI:
KUREJESHWA
KWA SH. 10,000,000/= ZILIZOCHUKULIWA KWA UTARATIBU WA MIKOPO INAYOUMIZA
WAKOPAJI
Mnamo tarehe 21.05.2020 Ofisi
ya TAKUKURU Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza ilipokea taarifa kutoka kwa
Mwalimu Mstaafu aitwaye AUGUSTINE JOSEPH NGOWI kuwa amedhulumiwa mafao yake ya
kustaafu na mtu aitwaye EMMANUEL DANIEL CHACHA Mkazi wa Misungwi - Mwanza.
Taarifa ilidai kwamba
mwalimu huyo baada ya kustaafu na kulipwa mafao yake ya zaidi ya sh milioni 95
- jumla ya shs milioni 14,900,000/= zilichukuliwa kwenye akaunti yake na
mlalamikiwa kwa njia isiyo halali.
1.0 UCHUNGUZI
Uchunguzi
wa TAKUKURU Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza ulianzishwa na kubaini yafuatayo:
· Mwl
Augustine Joseph Ngowi (62) alikuwa mtumishi wa umma- Mwalimu Mkuu katika Shule
ya Msingi Mwanangwa iliyopo wilayani Misungwi Mkoa wa Mwanza.
· Mwalimu
Ngowi alistaafu kwa lazima mnamo tarehe 12.12.2018 na kulipwa mafao yake ya
kustaafu na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii – NSSF ( Kwa sasa PSSSF) tarehe 17.04.2019.
· Uchunguzi
umebaini pia kwamba Mwl Augustine Joseph Ngowi alikopa fedha kwa EMMANUEL DANIEL CHACHA (32) kiasi cha Sh
3,490,000/ kwa kipindi cha kuanzia Novemba 2018 hadi April 2019 ambapo
walikubaliana kulipana mkopo huo kwa riba ya 20% kwa kila mwezi.
· Fedha
aliyokopeshwa alipewa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza alipewa sh 390,000/= CASH
mwezi Novemba 2018, aidha tarehe 24 Disemba 2018 aliwekewa sh 1,000,000/-
kwenye akaunti yake ya benki ya NMB Akaunti namba 31308000647, Tarehe 13
Februari 2019, alikopa sh 600,000/ ziliingizwa kwenye akaunti yake, na tarehe
11 Machi, 2019 alikopa sh 300,000/ nazo ziliingizwa kwenye akaunti yake na mwisho
ni tarehe 10 April 2019 alikopa sh 1,200,000/ nazo ziliingizwa kwenye akaunti
yake, hivyo jumla ya fedha yote aliyokopa ni sh 3,490,000/-. Wakati
wanakopeshana walisainishana mkataba ambao hata hivyo mkataba huo ulichanwa
baada ya mlalamikiwa kuchukua fedha kiasi cha sh 14,900,000/- baada ya mafao ya
mstaafu huyo kutoka.
· Mlalamikiwa
baada ya kutoa mkopo alishikilia kadi ya benki ya mkopaji pamoja na namba ya
siri ambapo alikuwa akitumia kadi hiyo
kuangalia salio mara kwa mara kwenye akaunti ya mkopaji ya Mwl Augustine Joseph
Ngowi.
· Mnamo
tarehe 17.04.2019 Mwl Augustine Joseph Ngowi alipokea mafao yake ya kustaafu ambapo
fedha ziliwekwa kwenye akaunti yake.
· Baada
ya kukuta kuna fedha alimjulisha mwalimu Augustine Joseph Ngowi ambapo alimtaka
afike Misungwi ili aweze kutoa fedha na kulipa mkopo huo. Tarehe 24.4.2019
mwalimu Augustine Joseph Ngowi alifika kwa Emmanuel Daniel Chacha ambapo mkopeshaji
huyo alimwacha mwalimu huyo nyumbani na kwenda kwa wakala wa NMB na kuhamisha
kiasi cha Tsh 14,900,000/-.
· Kati
ya fedha hizo kiasi cha Sh. 14,000,000/- kiliwekwa kwenye akaunti ya Hamis
Daniel Marwa akaunti namba 50710008439 ya NMB ambaye ni mdogo wake mkopeshaji, na Tsh 900,000/- aliziweka kwenye
akaunti yake yeye mwenyewe Emmanuel
Daniel Chacha akaunti namba 313110009120 NMB.
Baada
ya uchunguzi wa kina kufanyika na kubaini ukweli wa malalamiko haya, Bw
Emmanuel Daniel Chacha alikiri kuchukua fedha hizo na akaagizwa kuzirejesha
mara moja.
Tayari
fedha hizo kiasi cha sh 10,000,000/= zimerejeshwa ili akabidhiwe Mwl Augustine
Joseph Ngowi.
WITO:
Ninawataka wakopeshaji wote katika Wilaya hii ya
Misungwi kufuata taratibu na sheria ikiwemo kujisajili katika vyombo husika vya
Serikali na kufanya biashara hiyo wakiwa na leseni halali huku wakilipa mapato
ya Serikali vinginevyo Serikali hususani TAKUKURU
itawachukulia
hatua za kisheria.
Aidha
ni vema wakopaji wote hususani wastaafu wanaosubiri kulipwa mafao yao, wote
wakaepuka mikopo umiza yenye riba kubwa.
2.0
KUREJESHWA KWA SHS 1,227,000/= KUTOKANA NA MRADI WA UJENZI WA MABOMA SHULE YA
SEKONDARI IGOKELO.
1.1
UTANGULIZI:
Ofisi ya TAKUKURU wilaya ya misungwi mkoani
Mwanza kupitia moja ya majukumu yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo
ilifanikiwa kuokoa kiasi cha sh 1,227,000/= katika mradi wa ukamilishaji wa maboma
ya Shule ya Sekondari IGOKELO. Katika mradi huo kila kijiji kilitakiwa kujenga
boma lake na mradi huo uliojumuisha jumla ya vijiji sita.
2.2 UCHUNGUZI:
Uchunguzi wa
TAKUKURU Wilaya ya Misungwi ulibaini kwamba:
·
Kijiji cha Busolwa kilishindwa kukamilisha
boma lake kutokana na
usimamizi mbovu wa fedha zilizokusanywa.
·
Jumla ya fedha zilizokusanywa katika kijiji
cha Busolwa ni sh 4,160,500 na
zilizotumika zilikuwa sh 2,933,500 na
hivyo kufanya jumla ya fedha zilizopotea kuwa sh 1,227,000/=
·
Viongozi wa vijiji na kata ndiyo waliokuwa
wanahusika katika usimamizi wa fedha
zote zilizokusanywa kutoka kwa wananchi na wao ndiyo waliofanya matumizi
mabaya ya hizo fedha, hivyo ofisi ya TAKUKURU (W) Misungwi iliwataka viongozi
wote waliohusika kuzirejesha fedha hizo sh
1,227,000/= mara moja katika ofisi ya TAKUKURU wilaya ya Misungwi na tayari
fedha hizo zimerejeshwa ili zipelekwe katika ujenzi wa mradi husika ambao ni
kumalizia darasa lililotakiwa kujengwa na kijiji cha Busolwa.
3.0 KUREJESHWA KWA TSHS 7,050,000/= ZA MAKUSANYO
YA MAPATO KWA KUTUMIA MASHINE ZA KI
ELEKTRONIKI (POS) KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MISUNGWI
3.1 UTANGULIZI:
Ofisi ya TAKUKURU (W) Misungwi kwa kushirikiana na Jeshi
la Polisi imeokoa kiasi cha fedha sh 7,050,000/=
zilizokusanywa kwa kutumia mashine za kukusanyia mapato lakini hazikuwasilishwa
Benki kwenye akaunti ya kukusanyia mapato ndani ya Halmashauri.
3.2
UCHUNGUZI:
Uchunguzi wa TAKUKURU Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza
umebaini kwamba:
· Fedha
hizo walikuwa wanadaiwa wakusanya mapato waliokuwa wanakusanya mapato kwa
kutumia Point of sale (POS) mashine.
· Mapato
yaliyokuwa yanakusanywa ni ya kipindi cha mwaka 2018/2019 na walishindwa
kuwasilisha Benki katika akaunti ya Halmashauri ya wilaya ya Misungwi.
· Ofisi
ya TAKUKURU (W) Misungwi kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi iliwatafuta
wadaiwa wote walioshindwa kuwasilisha fedha Benki na kuwataka kurejesha fedha
hizo zenye jumla ya Tsh 7,050,000/=.
· Tayari kiasi cha shilingi 725,000/=
zimeshawekwa Benk na kiasi cha sh 6,325,000/= leo zinakabidhiwa ili
zipelekwe Benki katika akaunti ya Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi.
WITO:
Ofisi ya TAKUKURU Wilaya ya Misungwi kwa
kipindi cha mwezi Juni 2020 imeokoa jumla ya kiasi cha shilingi 18,277,000/= ambazo zote leo zimekabidhiwa
kwa wahusika mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Misungwi.
EMMA
MWASYOGE
MKUU
WA TAKUKURU WILAYA YA MISUNGWI
KNY:
MKUU WA TAKUKURU (M) MWANZA
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇