Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Julai, 2020 amemteua Bw. Gabriel Pascal
Malata kuwa Wakili Mkuu wa Serikali (Solicitor
General)
Kabla ya uteuzi huo Bw. Malata alikuwa Naibu
Wakili Mkuu wa Serikali na anachukua nafasi ya Dkt. Julius Clement Mashamba.
Wakati huo huo,
Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Boniface Luhende kuwa Naibu Wakili Mkuu wa
Serikali (Deputy Solicitor General).
Kabla ya uteuzi huo, Dkt. Luhende alikuwa Mhadhiri
katika Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua nafasi
ya Bw. Gabriel Pascal Malata ambaye ameteuliwa kuwa Wakili Mkuu wa Serikali.
Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo tarehe
10
Julai, 2020.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇