Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 09 Julai, 2020 amefanya
uteuzi wa Mkuu wa Wilaya 1 na Mkurugenzi Mtendaji 1, kama ifuatavyo;
Kwanza, Mhe. Rais
Magufuli amemteua Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Advera
John Bulimba kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora.
Kabla ya uteuzi huo, ACP Advera
John Bulimba alikuwa Kamanda wa Kikosi cha Polisi TAZARA na anachukua nafasi
Bw. Godfrey William Ngupula.
Pili, Mhe. Rais
Magufuli amemteua Bw. Solomon Isack Shati kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara.
Kabla ya uteuzi huo, Bw. Solomon
Isack Shati alikuwa Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani
Katavi na anachukua nafasi ya Bw. Bryceson Paul Kibasa.
Wakati huo huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Kept (Mst)
George Huruma Mkuchika kwa mamlaka aliyokasimiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya 2, kama ifuatavyo;
Kwanza, amemteua
Bw. Omary Mwanga kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi.
Bw. Omary Mwanga anachukua nafasi
ya Bi. Husna Juma Sekiboko.
Pili, amemteua
Bw. Saitoti Zelothe Stephen kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbeya Mkoani Mbeya.
Kabla ya uteuzi huo Bw. Saitoti
Zelothe Stephen alikuwa Afisa Tarafa Wilayani Mbulu katika Mkoa wa Manyara na
anachukua nafasi ya Bw. Hassan M. Mkwawa.
Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo
tarehe 09 Julai, 2020.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chamwino
09
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇