Kaimu Afisa Mkuu wa Fedha wa NMB, Benedicto Baragomwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakiwa wameshika madawati yaliyokabidhiwa na benki ya NMB kwa ajili ya shule saba za jijini Tanga kwenye hafla ya makabidhiano yaliyofanyika katika shule sekondari Pongwe nje kidogo ya Jiji la Tanga. Kutoka kushoto ni Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini - Aikansia Muro, Katikati mwenye miwani ni Meneja wa NMB Madaraka, Elizabeth Chawinga na Mwisho kulia ni Mkurugenzi wa jiji la Tanga, David Mayeji.
Benki ya NMB imetoa msaada wenye
thamani ya shilingi Milioni 36 kwa shule Saba za sekondari; Kirare, Japan,
Chongoleani, Nguvumali, Pongwe na Galanos za Jijini Tanga, kwa kuzipatia madawati
250 pamoja na mabati 352 ili kutatua changamoto za kielimu.
Akikabidhi msaada huo katika
shule ya sekondari ya Pongwe kwa Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee
na Watoto, Ummy Mwalimu, Kaimu Afisa Mkuu wa fedha wa benki hiyo - Benedicto
Baragomwa alisema, wamekuwa mstari wa mbele kushiriki kwenye miradi mbalimbali ya
maendeleo kwa wananchi.
Alisema kwa upande wa sekta ya
elimu, kipaumbele wamekiweka kwenye madawati, vifaa vya kuezekea huku kwenye
afya wakitoa vifaa vya tiba kama vitanda vya kujifungulia wakina mama na vitanda
vya wagonjwa na magodoro yake vilevile na kusaidia majanga yanayoipata nchi.
Aidha aliongeza kuwa, katika
kipindi cha miaka minne benki hiyo imekwisha changia zaidi ya shilingi Bilioni
nne kusaidia jamii katika ununuzi wa vifaa tiba 330 kwa hospitali na vituo vya
Afya, zaidi ya madawati 31,150 pamoja na kompyuta1,150 nchi nzima.
"Kwa mwaka huu NMB imetenga
zaidi ya shilingi Bilioni moja kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamii
ikiwemo kusaidia sekta ya afya na elimu" alisema Baragomwa.
Kwa upande wake Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema kuwa elimu
bure imeweza kusaidia watoto wengi wa kike kupata fursa ya elimu tofauti na
hapo awali.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇