Msemaji wa Familia ya
Mkapa,Bw.William Urio amesema wanatoa shukrani kwa Serikali ambavyo
imekuwa pamoja nao na kushughulikia Msiba huu na wanavyoendelea
kushughulikia,wanashukuru kwa uamuzi wa kuanza shughuli za kuaga kwa
Misa Takatifu,tunawashukuru Maaskofu kwa kukubali kuendesha Misa.
”Mzee Mkapa alikuwa
hajisikii vizuri akaenda Hospitali akaonekana alikuwa na Malaria akaanza
matibabu akalazwa Jumatano, Alhamisi mchana aliendelea vizuri nilikuwa
naye hadi saa mbili alikuwa anaangalia Live ya chaguzi za wagombea Ubunge
Viti Maalum CCM” Msemaji wa Familia ya Mkapa, Bw.William Urio.
Aidha Msemaji wa
Familia ya Mkapa, Bw. William Urio,amesema kuwa Mzee Mkapa siku ya
Alhamisi usiku baada ya kutazama LIVE ya chaguzi Viti Maalum akasikiliza
taarifa ya habari, baadaye aliinuka akitaka kutoka akakaa akainamisha
kichwa, walipokuja kumpima wakathibitisha kuwa amefariki, sababu ya kifo
cha Mzee Mkapa ni mshtuko wa moyo.
#RIPMzeeMkapa
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇