Mkuu wa Wilaya ya Magu, Salum
Kalli, akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji
cha Shishani baada ya kukgua miradi y maendeleo ya ujenzi wa jengo la
RCH na nyumba za waganga katika Zata ya Shishani jana.Picha na Baltazar
Mashaka
…………………………………………………………………………………..
NA BALTAZAR MASHAKA,MAGU
MKUU wa Wilaya ya Magu, Salum
Kalli, akikagua shughuli na miradi ya maendeleo amekumbana na kero ya
wananchi wa Kijiji cha Nyasato, Kata ya Jinjimili wakilalamikia
kushambuliwa na fisi hali inayotishia usalama na maisha yao.
Walitoa kilio hicho kwa mkuu huyo
wa wilaya kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo jana
baada ya kukagua shughuli na miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta
za afya, elimu na maji.
Mmoja wa wananchi hao Maira Sanga
akizungumza kwa niaba ya wenzake alisema kuwa, maisha yao yako hatarini
pamoja na familia zao kutokana na kushambuliwa fisi na hivyo kujenga
hofu kwa wananchi wa kijiji hicho.
“Mheshimiwa mkuu wa wilaya hapa
tunakabiliwa na tatizo la wanyama wakali aina ya fisi wanatishia uhai
na maisha yetu pamoja na familia.Wanyama hao wamekuwa tishio kwenye
jamii kutokana na kuwashambulia na kusababisha washindwe kufanya
shughuli za uzalishaji,tunaomba serikali itusaidie kuwakabili na
kuwapunguza,”alisema Sanga.
Alisema hivi karibuni kijana mmoja
alishambuliwa na kung’atwa fisi mguuni, familia moja nayo ilivamiwa
usiku na fisi hao, pia wanyama hao waliwahi kuwashambulia watoto watatu
wakiwa njiani kuelekea shuleni na kusababisha vifo vyao hivyo wamekuwa
tishio kwa maisha ya wananchi na wakazi wa Kijiji cha Nyasato .
Akijibu kilio cha wananchi hao
Kalli alisema atatoa kibali cha kuwapunguza ili wasiendelee kuleta
madhara kwenye jamii na akatoa angalizo kuwa wasilalamike kuwa
amepunguza nguvu kazi yao ya mashambani, hatawaelewa na wala serikali
haitaki wananchi walalamike.
“Ndugu zangu na watani wangu
Wasukuma tuwe wakweli, tukisha wapunguza mkilalamika baada ya zoezi hilo
kuwa nimepunguza wafanyakazi wenu wa mashambani sitawaelewa,tutanaka
watu wahangaike na mambo ya msingi si haya yanayohusu fisi,” alisema
Kalli na kumwagiza Mkuuwa Polisi Wilaya ya Magu Mahamoud Banga
kushirikiana na maofisa wa wanyamapori kutekeleza agizo.
Aidha Mrakibu huyo wa Mwandamizi
wa Polisi aliwaambia wananchi hao kuwa zipo taratibu za kuwashughulikia
wanyamapori wnaodhuru watu ingawa jeshi hilo haliamini ufugaji wa
wanyama unaodaiwa kufanywa na kabila la Wasukuma.
“Kama mnawafuga wanyama hao
(fisi) angalieni namna ya kuwahudumia lakini si kwa kuwalisha binadamu
na atakayebainika atachukuliwa hatua .Pia tuchunguze fisi hao wanaishi
na wanapatikana wapi na Afisa Mtendaji awasiliane na Ofisa Wanyamapori
waje kuwapunguza fisi hao,”alisema Banga.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇