Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB Dk. Edwin P. Mhede, akikabidhiwa Tuzo ya Benki Bora na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB- Ruth Zaipuna. Akishuhudia ni Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB – Filbert Mponzi
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB Dk.Edwin P. Mhede, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB- Ruth Zaipuna na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa NMB – Filbert Mponzi wakiifurahia Tuzo walioipokea kwa kuwa Benki Bora Tanzania.
Benki ya NMB imekuwa benki bora nchini Tanzania kwa mara ya nane mfululizo baada ya kuzibwaga benki zingine 40 nchini.
Benki ya NMB imekuwa benki bora nchini Tanzania kwa mara ya nane mfululizo baada ya kuzibwaga benki zingine 40 nchini.
Tuzo hiyo
imetolewa na Euromoney, ambalo ni jarida la kimataifa la masuala ya kifedha
linaloongoza duniani lenye makao makuu yake jijini London, Uingereza.
Tuzo hii
inaonesha kuwa Benki ya NMB ni zaidi ya taasisi inayotoa huduma za kifedha na
kuwa kichocheo muhimu cha mabadiliko ya kiuchumi kupitia utoaji huduma za
kibenki kwa njia ya kidigitali.
Akiongea wakati
wa kukabidhiwa tuzo hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya NMB – Dk.
Edwin Mhede alisema baada ya Tanzania kufikia uchumi wa kati, Benki ya NMB
inaahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu ili kuchangia zaidi katika
ukuaji wa uchumi kwenda katika hatua ya juu zaidi.
Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB - Ruth Zaipuna alisema:
“Leo hii tunajulikana kama benki imara
zaidi, yenye huduma za ubunifu wa kiteknolojia. Tumedhamiria kuwa zaidi ya
taasisi ya huduma ya fedha kwa kuendelea kuchochea mabadiliko ya kiuchumi
katika nchi yetu na kuboresha maisha ya Watanzania wenzetu kwa kutoa huduma zinazowafaa
na kukidhi mahitaji na mipango yao.”
Tuzo hiyo
hutolewa kwa kuzingatia vigezo kadhaa kwa benki zilizopendekezwa ukiwamo
ufanisi wa hesabu za fedha na utendaji kwa ujumla, mkakati wa huduma za
kidijitali, huduma jumuishi za fedha, usalama wa huduma za kimtandao na wajibu
wa benki kwa jamii inayoihudumia.
Vigezo vingine vilivyotumika ni mtaji wa
benki, mapato yatokanayo na biashara ya hisa, mapato yatokanayo na mali za
kampuni, pato litokanalo na riba, uwiano wa fedha na gharama za uendeshaji, kiwango
cha amana za wateja, Kiwango cha Mikopo katika soko, Uwiano kati ya mikopo na
amana za wateja, uwiano wa mikopo chechefu, uwiano wa hasara itokanayo na
mikopo chechefu.
Akizungumzia mchakato wa kumpata
mshindi wa tuzo ya benki bora nchini, mhariri wa Jarida la Euromoney, Clive
Horwood alisema: “Tunaendelea kuzitambua
taasisi bora zaidi katika kila nchi zinazotoa huduma za fedha. Kwa kila mwaka,
ukubwa ni muhimu lakini sio kigezo muhimu zaidi. Faida ya benki husika ni
muhimu kama ilivyo uwezo wa kuthibitisha uwezo wa kukua, ufanisi wa kiutendaji
ikilinganishwa na washindani wake sokoni na uwezo wa kukabili mazingira ya soko
yanayobadilika pamoja na kukidhi mahitaji ya wateja.”
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇