Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia jambo wakati akirejesha fomu za kugombea tena ubunge wa Jimbo la Ruangwa kwenye ofisi ya CCM ya wilaya ya Ruangwa baada ya kuzichukua na kuzijaza Julai 15, 2020. Kushoto ni Mkewe Mary Majaliwa.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa leo (Jumatano, Julai 15, 2020) amechukua fomu ya kuwania tena
ubunge wa jimbo la Ruangwa, wilayani humo, mkoani Lindi.
Waziri
Mkuu ambaye alizijaza fomu hizo akiwa ofisini hapo na kuzirudisha kwa Katibu wa
CCM wa Wilaya ya Ruangwa, Bw. Barnabas Essau, pia alilipa fedha taslimu sh.
100,000 zikiwa ni ada ya kuchukua fomu hizo.
Waziri
Mkuu aliambatana na mkewe Mama Mary Majaliwa.
Chama
Cha Mapinduzi (CCM) kilitoa ratiba ya kuwapata wagombea ubunge, udiwani na viti
maalumu kwa ajili ya uchanguzi mkuu wa mwaka 2020 ambapo wagombea wa nafasi
hizo walitakiwa kuchukua fomu kuanzia Julai 14, 2020 na kuzirejesha Julai 17,
mwaka huu saa 10.00 jioni.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATANO,
JULAI 15, 2020.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇