Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akizungumza na timu ya maafisa wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati walipomtembelea ofisini kwake kuzungumzia
kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendelea jijini hapa.
Afisa Msimamizi Mkuu wa Kodi Bi. Rose Mahendeka kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella kuhusu kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendelea jijini hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akiwa katika picha ya pamoja na timu ya maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati walipomtembelea ofisini kwake kuzungumzia kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendelea jijini hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendelea jijini hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendelea jijini hapa.
Afisa Msimamizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Patrick Massawe akimuelimisha Mfanyabiashara wa eneo la Lumumba mkoani Mwanza kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu kodi wakati wa Kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendelea jijini hapa.

Afisa Msimamizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Patrick Massawe akimuelimisha Mfanyabiashara wa eneo la Karuta mkoani Mwanza kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu kodi wakati wa Kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendelea jijini hapa.
Na Veronica Kazimoto
Mwanza
16 Juni,2020
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Mhe. John Mongella amewataka wafanyabiashara kutumia fursa ya kampeni ya elimu
kwa mlipakodi inayoendelea mkoani hapa kulipa kodi kwa wakati ili kuiwezesha
Serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo huku wafanyabiashara hao
wakiishukuru Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa zoezi hilo ambalo linawaleta
karibu walipakodi na wakusanya kodi.
Akizungumza na waandishi
wa habari kuhusu kampeni hiyo ambayo imeanza June 15 hadi 22 mwaka huu, Mkuu wa
Mkoa huyo amesema kuwa, ni muhimu wafanyabiashara wote wakalipa kipaumbele
suala la ulipaji kodi kwa wakati ili kuiwezesha Serikali kugharamia huduma za
jamii kwa manufaa ya kila Mtanzania.
“Kama mnavyojua umuhimu
wa kodi na hasa katika kipindi hiki cha awamu ya tano hakuna Mtanzania ambaye
hajashuhudia umuhimu wa kodi, tumeona barabara zikijengwa, ndege zikinunuliwa,
ujenzi wa vituo vya afya, meli zikijengwa, ukarabati wa viwanja vya ndege
ambavyo vyote vimesababishwa na uwezo wa serikali ambao umejengeka kwa mapato
ya ndani,” alisema Mhe. Mongella.
Mhe. Mongella amesema
kwamba, kutokana na faida hizo za kodi, ni muhimu wafanyabiashara wote wakatoa
ushirikiano kwa maafisa hao wa TRA watakaopita katika maeneo ya biashara zao wakifanya
zoezi hili la kutoa elimu ya kodi na kutumia fursa hiyo kupata uelewa na hatimaye
waweze kulipa kodi ipasavyo na kwa wakati.
Amesema zoezi hilo
limelenga kuwafikia wananchi na wafanyabiashara wa maeneo mbalimbali mkoani
hapa yakiwemo Rwagasore, Pamba road, Buhongwa, Nyerere road, Misungwi, Mwaloni
na Kisesa.
Sambamba na hayo amesema
mambo yote yamefanikiwa kutokana na uadilifu na utendaji kazi wenye tija
uliofanywa na serikali ya awamu ya tano katika kusimamia mapato ya ndani na
kuyaelekeza katika kuimarisha uchumi wa nchi.
Frola Ayo ambaye ni
mfanyabiashara wa mapambo na Charles Lyamuya mfanyabiashara wa duka la vifaa
vya ujenzi ni baadhi ya walipakodi waliopo Mtaa wa Lumumba na Karuta jijini
hapa ambapo wameomba zoezi la utoaji elimu kwa mlipakodi liwe endelevu kwani
linajenga urafiki baina yao na TRA na hivyo litaongeza uhiari wa kulipa kodi
kwa wakati.
"Kutokana na elimu
hii hakika tutalipa kodi ipasavyo kwa sababu inatuweka karibu na TRA suala
ambalo linatuondolea hofu na pia tunaomba elimu hii iwe endelevu ili
wafanyabiashara wengi waweze kujijenga zaidi na kuimarika katika biashara zao,”
alisema Lyamuya.
Kampeni ya elimu kwa
mlipakodi inayoendelea mkoani Mwanza inafanyika pia katika Mkoa wa Morogoro na
Mbeya na imelenga kuwaelimisha walipakodi juu ya mambo mbalimbali yanayohusu
kodi ikiwa ni pamoja na kupokea maoni, kusikiliza kero na changamoto za
walipakodi hao ili kuzitafutia ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇