LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 27, 2020

SIKU YA KUPINGA VITA DAWA ZA KULEVYA

   Wakati Tanzania ikiadhimisha siku ya kimataifa ya kupiga vita dawa za Kulevya, kwa kipindi cha takribani miaka mitano Tanzania imefanikiwa kupunguza uingizwaji wa dawa za kulevya kwa asilimia 90 huku zaidi ya watuhumiwa elfu 70 wakikamatwa.
Akizungumizia maadhimisho hayo na mafanikio yaliyopatikana Waziri wa nchi ofisi ya waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na wenye ulemavu Jenista Mhagama anasema mafanikio hayo yamepatikana baada ya kubaini na kuvunja mitandao hiyo hapa nchini kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kimataifa.

Pamoja na kazi hiyo iliyofanywa na serikali kwa kushirikiana nan chi mbalimbali na taasisi za kimataifa ili kudhibiti uingizwaji wa dawa hizo hapa nchini bado Dawa zinazozalishwa hapa nchini zinaonekana kuwa changamoto.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages