LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jun 27, 2020

DKT. BASHIRU AHIMIZA HAKI KWA WATENDAJI WA CCM WILAYANI

  Katibu Mkuu wa Chama ca Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally amewatahadharisha makatibu wa chama hicho ngazi ya Wilaya kujiepusha na vitendo vya rushwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu ili kutenda haki kwa kila mwanachama anayetaka kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.
Dkt. Bashiru ameeleza hayo wakati akifungua semina ya mafunzo kwa makatibu wa CCM ngazi ya wilaya kote nchini na kuonya kuwa miongoni mwa mambo yanayovunja haki ni rushwa na kuwataka makatibu hao kusimamia haki kwa kutojihusisha na vitendo vya rushwa.

Mambo mengine aliyosisitiza Dkt. Bashiru ni Pamoja na watendaji hao kusimamia nidhamu ndani ya chama, haki na kuwapa motisha wana CCM wenye moyo wa kujitolea.

Awali akimkaribisha katibu mkuu kwa ajili ya ufunguzi wa semina hiyo, Naibu katibu mkuu wa CCM Bara Rodrick Mpogolo akawataka watendaji hao kuhakikisha wanaongeza asilimia za ushindi kwa CCM ili chama kijiongezee kiwango cha ruzuku kutokana na asilimia za ushindi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages