Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirila la Nyumbu Brigedia Jenerali Hashim Komba (kushoto) wakisaini hati ya makubaliano kati ya TPA na Shirika la Nyumbu kwa ajili ya kuendelea kutengeneza terminal treila na kufanya ukarabati wa terminal treila zilizoharibika.Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ,Jenerali Venance Mabeyo (katikati), Mwenyekiti wa Bodi ya TPA Profesa Ignas Rubaratuka na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Nyumbu Balozi Luteni Jenerali mstaafu Wyjones Kisamba(kushoto).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko (kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Shirila la Nyumbu Brigedia Jenerali Hashim Komba (kushoto) wakiwa wameshika hati ya makubaliano ya Nyumbu kuendelea kutengeneza na kukarabati vitendea kazi vya TPA ikiwemo terminal treila kwa ajili a kubebea makontena.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akizungumza leo jijini Dar es Salaam kabla ya Shirika la Nyumbu Tanzania kukabidhi terminal treila(tela la kubebea makontena) kwa Mamalaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) .Tela hizo zimetengenezwa na shirika la Nyumbu.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko akizungumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu uamuzi wa TPA kuamua kutumia Shirika la Nyumbu kwa ajili ya kutengeneza terminal treila kwa ajili ya kubebea makontena bandarini hapo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) Profesa Ignas Rubaratuka akifafanua wakati wa ghafla ya ukabidhiwaji wa terminal treila(tela za kubebea makontena) ambayo yametengenezwa na Shirika la Nyumbu na kisha kukabidhi kwa TPA.
Viongozi wa ngazi mbalimbali wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) pamoja na maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venancy Mabeyo wakiwa kwenye tukio la makabidhiano ya treila za kubebea mankotena yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumbu Brigedia Jenerali Hashim Komba akitoa ufafanuzi kuhusu terminal treila ambazo wamezitengeneza na kisha kukabidhi kwa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA).
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) na Shirika la Nyumbu baada ya kufanyika kwa makabidhiano ya terminal treila.Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wa kada mbalimbali wa TPA na maofisa wa JWTZ.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) Mhandisi Deusdedit Kakoko(wa pili kulia) akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo.
Moja ya Terminal Treila (tela za kubeba makontena) likiwa katika Bandari ya Dar es Salaam.Treila hilo ni miongoni mwa treila ambazo zitafanyiwa matengenezo kurudisha kwenye ubora wake na Shirika la Nyumbu. (PICHA ZOTE NA SAID MWISHEHE).
Said Mwishehe, Michuzi TV
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) kupitia Shirika la Nyumbu wameshirikiana na kufanikisha mchakato muhimu wa utengenezaji Vichanja (terminal trailers) vya kubebea mizigo na hasa makontena katika Bandari ya Dar es Salaam.
Tukio hilo la makabidhiano limefanyika leo Juni 6,2020 na kushuhudiwa na viongozi wa wa TPA, wafanyakazi wa mamlaka hiyo pamoja na maofisa wa ngazi mbalimbali kutoka JWTZ wakiongozwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Venancy Mabeyo.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mhandisi Deusidedit Kakoko amesema kukamilika kwa kazi hiyo kunaongeza kasi ya uvutaji wa makasha na ufanisi wa kazi za kupakia na kupakua mizigo bandarini. Aidha, ushirikiano huo wa TPA na JWTZ kupitia Shirika la Nyumbu ni uthibitisho wa utekelezaji wa maelekezo ya Serikali kwa taasisi zake kujengeana uwezo na kushirikiana katika kuwahudumia wananchi.
"Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ilingia mkataba na Shirika la Nyumbu linalomilikiwa na Wizara ya ulinzi na jeshi la Kujenga taifa(JKT)Mei 23,2019. Mkataba huo uliipatia Nyumbu kandarasi ya kutengeneza vichanja (terminal trailers) vitano (5) kwa ajili ya Bandari ya Dar es Salaam kwa thamani ya Sh. 524,260,000."Katika mkataba huo, Shirika la Nyumbu lilikuwa na majukumu kadhaa ili kukamilisha utengenezaji wa 'trailers' hizi. Majukumu hayo ni pamoja na usanifu na utayarishaji wa michoro ya trailers, kufanya tathmini ya upatikanaji wa malighafi, usanifu na ukataji wa vyuma, kufunga vifaa vya breki na umeme pamoja kupiga rangi.
"Vichanja (terminal trailers) hizi zilikabidhiwa kwa TPA Machi 15, na Machi 17, 2020 ukaguzi wa mwisho kwa ajili ya kukabidhi mradi. Kwa sasa vichanja hivi vipo katika muda wa uangalizi wa mwaka mmoja. Sote tunajionea kazi nzuri iliyofanyika katika muda mfupi, kwa ubora wa hali ya juu sana na kuokoa kiasi kikubwa cha fedha za kigeni ambazo zingetumika kuagiza vichanja hivi kutoka nje ya nchi,"amesema Mhandisi Kakoko.
Ametoa mwito kwa taasisi nyingine za umma na hata zile za binafsi zinazopata fursa ya kufanya kazi na TPA, kuzingatia gharama halisi na muda uliowekwa katika kutekeleza kazi zao. "Naomba kutumia fursa hii kurudia kutoa mwito kwa wateja na wadau wa sekta ya bandari kuendelea kuzitumia bandari zetu kote nchini sambamba na kuitunza miundombinu yake kwa faida ya sasa na siku zijazo".
Kwa upande wake MKUU wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo amesema anatoa shukrani kwa uongozi wa Shirika la Nyumbu na TPA kwa kupata fursa ya kushuhudia makabidhiano ya vifaa hivyo ambavyo vimetengenezwa na Nyumbu."Ni tukio la kihistoria taasisi moja kufanya kazi na taasisi nyingine, kumekuwa na tabia ambayo imejengeka kuwa muda mrefu wa kuamini vinavyotengenezwa nje ni bora zaidi kuliko vinavyotengenezwa hapa hapa nchini.
"Natoa shukrani kwa uongozi wa bandari kwa kutuamini na kutupa kazi ya kutengeneza vichanja hivi na tunajisikia fahari tunaposhirikishwa kujenga uchumi wa nchi kwa kushirikiana na taasisi nyingine. Jeshi la Wananchi wa Tanzania linaonesha namna ambavyo linaweza kufanya mambo mengi , kuna vijana wengi wasomi na watalaam walioko jeshini ambao wanao uwezo mkubwa wa kufanya mambo makuwa,"amesema.
Jenerali Mabeyo amesema kuwa fursa ambayo wameipata ni changamoto ya kuongeza jitihada katka utendaji kazi wao wa kila siku, huku akitumia nafasi hiyo kueleza kuwa watalimarisha shirika la Nyumbu ikiwa ni pamoja na kuongeza askari."Nyumbu lilikuwa ni shirika la utafiti lakini sasa tunafanya tafiti na kisha tunazalisha. tunashukuru TPA kwa ushirikiano ambao tumekuwa tukiupata wakati wote."
Wakati huo huo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA Profesa Ignas Rubaratuka amesema kwa kipekee wanamshukuru Mkuu wa Majeshi kwa kutenga muda wake na kushuhudia makabidhiano hayo ya kazi nzuri iliyofanywa na vijana wazalendo ambao wamethibitisha kuwa pamoja na weledi uliotukuka katika shughuli za ulinzi na usalama wa nchi yetu, lakini pia Jeshi letu ni kiungo muhimu katika kazi za fani mbalimbali zenye mchango mkubwa katika Ujenzi wa Taifa letu.
"Jumuia nzima ya TPA tumefurahishwa sana tukio hili na ubora wa Vichanja hivi. Kazi hii imefanyika kwa muda mfupi, kwa kutumia waataalamu wa ndani ya nchi yetu na gharama nafuu ambazo ni halisi. Hakika, ushirikiano huu ni ushahidi kuwa, taasisi za umma zikiamua kushikana mkono na kuwezeshana, matokeo yake huwezesha kufikiwa kwa malengo yaliyokusudiwa kwa wakati.
Pia amesema kazi nzuri iliyofanywa na Shirika la Nyumbu , TPA imeamua kusaini Mkataba wa ushirikiano (MoU) wa kipindi cha miaka mitatu(03) ili Jeshi letu Kikosi cha Nyumbu wafanye kazi nyingine ya kutengeneza Vichanja vipya na kukarabati vichanja chakavu vinavyotumika Bandarini.
"Tunaamini kuwa, kupitia ushirikiano huu na uwezo mkubwa wa Jeshi letu,kazi hii itafanyika kwa kuzingatia ubora, gharama nafuu na halisi. Tunawatakia kila jema katika kutekeleza kazi hii,"amesema.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇