LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

May 17, 2020

RAIS MAGUFULI: WAGONJWA CORONA NCHINI TANZANIA WAMEPUNGUASANA

  Rais John Magufuli amesema kuwa idadi ya wagonjwa wa Corona nchini Tanzania imepungua sana, huku baadhi ya vituo vilivyotengwa kwa ajili ya kuwahudumia wenye maambukizi vikiwa vitupu.

Rais amesema hilo wakati akitoa salamu kwa Watanzania alipohudhuria ibada ya Jumapili- KKKT Usharika wa Chato Mkoani Geita,

Akitoa takwimu hizo Rais Magufuli amesema kwa Mkoa wa Dar es Salaam;

Amana ilikuwa inalaza wagonjwa 198 leo walikuwepo watu 12 walioathirika, Mloganzila walikuwa watu 30 leo 6, Kibaha huwa wanalazwa watu zaidi ya 50 leo wamebaki watu 22 ambao hali zao ni nzuri.

Akitaja vituo vingine amesema Aga Khan wamebaki watu 31, Hindu Mandali wamebaki 16, Regency 17, TMJ wamebaki 7, Rabininsia wamebaki 14.

Katika mikoa mingine amesema, Arusha kuna vituo vitatu, Moshono kuna wagonjwa 11, Longido na Karatu hakuna mgonjwa.

Mwanza kuna vituo 10 ambapo Buswelu kuna wagonjwa 2, Misungwi 2 Ukerewe, Magu, Mkuyuni, Bachosa, Sengerema, Kwemba kote hakuna mgonjwa, huku Hospitali ya Bungando na Sékou Touré kuna wagonjwa 2 wenye uhitaji maalum.

Dodoma kuna vituo vinne ambapo mjini viko viwili kuna wagonjwa wawili huku Kongwa na Kondoa kukiwa hakuna hakuna mgonjwa.
“Mungu ametusaidia na kwa taarifa za leo wagonjwa wamepungua sana Amana ilikuwa inalaza Watu 198, leo walikuwepo Watu 12 tu, Mlogonzila ilikuwa inalaza Watu 30 leo wamebaki 6, pale Kibaha Hospitali ilikuwa inalaza zaidi ya Watu 50 leo wamebaki Watu 22”-JPM
View image on Twitter
See MPEKUZI's other Tweets



“Kwa hali hii, kama wiki tunayoianza kesho itaendelea hivi nimepanga kufungua vyuo ili Wanafunzi wetu waendelee kusoma, lakini nimepanga pia kuruhusu michezo iendelee kwasababu michezo ni sehemu ya Burudani, maisha lazima yaendelee” -JPM
View image on Twitter
See MPEKUZI's other Tweets



“Mimi Mtoto wangu wa kumzaa amepata corona akajifungia, akajifukiza akapiga malimao, sasa hivi ni mzima kabisa anapiga push-up, msije mkadhani mimi sijapata Mtu wa karibu mwenye corona, tuondoe hofu”-JPM
View image on Twitter
See MPEKUZI's other Tweets



“Sijaona umuhimu wa kufunga mipaka, juzi nimezungumza na Rais Museveni ametuuzia Tani za sukari Elfu 26, tungefunga mipaka tungepata hiyo sukari ya Uganda? , unakuta Dereva anazuiliwa sijui kwenda wapi? Wakati ametoka DSM hadi huko ametembea KM Elfu moja na kitu hajaanguka!” -JPM
View image on Twitter
See MPEKUZI's other Tweets



“Tanzania hakuna cha lockdown, wala Baba yake lockdown, wala Ndugu yake lockdown, tunaendelea kuchapa kazi wakimaliza kujilock huko watakuja tutawasaidia chakula, na tusiwabague, ndani ya Afrika Mashariki na SADC tuko pamoja lakini kila Mtu ana njia zake za kutatua tatizo” -JPM
View image on Twitter
See MPEKUZI's other Tweets



“Huwezi kuwa una mji wako halafu unapangiwa la kufanya, Mzee wetu wetu Kikwete alisema la kuambiwa changanya na lako, haiwezekani ukiambiwa jifungie,unajifungia chumbani wakati hauna chakula, tutaenda tunavyotaka, hili ni Taifa huru, Taifa linalojiamini, tumepambana na mengi”-JPM
View image on Twitter
See MPEKUZI's other Tweets

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages