Taarifa zinaeleza kuwa, washirika wa Rais Nicolas Maduro wa Venezuela na wale wa mpinzani wake, kiongozi wa upinzani Juan Guaido, wameanza mazungumzo ya siri wakati hofu imetanda nchini humo juu ya kuenea zaidi kwa virusi vya Corona.
Mazungumzo hayo yanafanyika wakati kuna wasiwasi mkubwa kuhusu janga la virusi vya Corona au COVID-19, mfumuko wa bei na uhaba wa mafuta na pia hofu kwa baadhi ya wafuasi wa chama tawala cha Kisoshalisti ambao wana wasiwasi juu ya jinsi ya kuendelea na maisha yao ya kisiasa ikiwa hakutakuwa na mabadiliko katika serikali huku serikali ya Washington ikiendelea kuongeza vikwazo vyake.
Mazungumzo haya yanaonesha kuwa washirika wa Maduro na wale wa Guaido hawaamini kuwa, kila upande unaweza kuushinda mwingine katika janga la kimataifa na vikwazo vya Marekani vinavyolenga kumshinikiza Maduro aondoke madarakani.
Hijajulikana ni lini mazungumzo hayo yalianza, wapi na jinsi gani yanafanyika, au upi mtazamo wa Maduro na Guaido kuhusu mazungumzo hayo.
Hivi karibuni Juan Guaido kiongozi wa upinzani nchini Venezuela alitoa wito wa kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa itakayowashirikisha wapinzani akieleza kwamba, hatua hiyo itafanikisha mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 nchini humo.
Mgogo wa Venezuela ulishadidi baada ya tarehe 23 Januari mwaka jana, Juan GuaidĂł, kiongozi wa upinzani kulijitangaza kuwa rais wa Venezuela akipata uungaji mkono wa wazi wa serikali ya Marekani na waitifaki wake, hatua ambayo ilitajwa na serikali na taifa hilo kuwa ni mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Rais Nicolas Maduro.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇