Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Giveness Aswile akielezea katika mkutano huo kuhusu tofauti ya Elimu ya Uraia na Elimu ya Mpiga Kura.
Baadhi ya viongozi wa siasa wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa NEC
Baadhi ya viongozi wa Asasi za Kiraia, wenye urevu, vijana wanawake na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Tume baada ya mkutano huo kumalizika
Katibu wa Chama cha AFP Mkoa wa Dar es Salaam, Ndonge Said Ndonge akichangia mada wakati wa mkutano huo, ambapo aliitaka Tume kuanzia sasa watu wenye ulemavu waache kuwaita wenye makundi maalumu bali waitwe Makundi yenye Mahitaji Maalumu. Tume ililidhia ombi hilo.
Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji, Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Novaita Mrosso akiwasilisha mada katika mkutano huo wadau wa uchaguzi kuhusu sifa za kuwa raia wa Tanzania.
Baadhi ya Wadau wakisikiliza kwa makini wakati Mkurugenzi wa NEC, akiwasilisha mada kuhusu uhamasishaji wa katika uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake na Watoto wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu Tanzania, Nasiriya Nasir Ally akichangia mada wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Wilson Charles Mahera akizungumza na wanahabari kuhusu yaliyojiri kwenye mkutano huo.
Na Richard Mwaikenda
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), tayari imekamisha zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika ikoa 23 Tanzania Bara na mikoa mitano ya Tanzania Zanzibar.
Mikoa iliyobakia ni Morogoro katika baadhi ya halmashauri na mikoa ya Dar es Salaam na Pwani
ambayo unatarajiwa kufanyika kwa siku saba, kuanzia Februari 14 hadi 20 mwaka
huu,
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano ulioikutanisha
tume ya Taifa ya uchaguzi na wadau wa uchaguzi wa Mkoa wa Dar es Salaam
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini, Jaji Semistocles Kaijage amesema
kuwa maandalizi kwa ajili ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu
la wapiga kura katika mikoa hiyo umekamilika na kuwataka wale wote wenye
sifa kutumia haki yao ya kikatiba kwa kujiandikisha ili kuweza
kushiriki katika katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu.
Amesema kuwa uboreshaji wa daftari la kudumu hautahusisha wapiga
kura wote walioandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura mwaka
2015.
"Uboreshaji
huu unawahusu wapiga kura wapya ambao wametimiza miaka 18 na wale ambao
watatimiza umri wa miaka 18 siku ya uchaguzi mkuu mwaka huu." Ameeleza.
Aidha amesema kuwa kwa wale ambao wamehama kutoka maeneo yao ya
awali na kuhamia maeneo mengine, wenye kadi zilizoharibika au kupotea na
wale wanaotakiwa kuondolewa kwenye daftari kwa sababu za kufariki au
kupoteza sifa watahusika katika maboresho hayo.
Vilevile amesema katika uboreshaji huo Kuna baadhi ya asasi za kiraia
ambazo zimepewa vibali vya kutoa elimu kwa mpiga kura kwa ajili ya
uboreshaji na kuwashauri wananchi kutumia nafasi hiyo kwa kujifunza
kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na amezitaka asasi
hizo ambazo zimepewa kibali na tume kutumia mwongozo wa utoaji wa elimu
ya mpiga kura uliotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi juu ya uboreshaji
wa daftari hilo.
Jaji Kaijage ametoa rai kwa wananchi wote kutunza kadi zao hadi siku
ya uchaguzi na hata baada ya uchaguzi kwa kuwa moja ya changamoto kubwa
iliyojitokeza katika baadhi ya maeneo yaliyokamilisha mchakato huo ni
pamoja na upotevu wa kadi, kadi kuharibika na wananchi kushindwa
kukumbuka majina yao hivyo kuchukua muda mrefu katika kutafuta majina
yao kwa usahihi.
Pia amesema wananchi wajitokeza mapema na sio kusongamana misururu
mirefu kwenye vituo vya kuandikisha wapiga siku za mwisho na kusema
kuwa hilo litafanikiwa ikiwa wadau, tume na wananchi watashirikiana
katika zoezi zima la uchaguzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Wilson
Charles Mahera amesema kuwa wananchi wenye sifa wajitokeze ili kutimiza
haki zao za kiraia na kueleza kuwa Tume inatambua mchango wa wadau
mbalimbali katika kuleta mabadiliko chanya na mwamko wa kimaendeleo
katika jamii yetu.
Amesema
kuwa Tume itaendelea kuzingatia Sheria na kanuni zake katika zoezi zima
la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na kuviomba vyama vya
siasa na wadau wengine kuzingatia Sheria za uchaguzi, kanuni za
uboreshaji na maelekezo kwa vyama vya siasa kuhusu zoezi la uboreshaji.
Mkutano huo umewakutanisha wajumbe wa Tume, viongozi wa vyama vya
siasa, dini, Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam, wawakilishi wa watu wenye
ulemavu, wanawake, vijana, asasi za kiraia na wahariri na waandishi wa
habari.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇