LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 7, 2020

MITAMBO YA KISASA YA UPASUAJI UBONGO BILA KUFUNGUA FUVU YATUA NCHINI, KUSIMIKWA MOI



NA ANDREW CHALE

TAASISI ya Tiba ya Mifupa (MOI) imeingiza nchini mitambo ya kisasa ya upasuaji wa Ubongo bila kufungua fuvu (Angio Suite) itakayokuwa msaada mkubwa katika tiba hapa nchini.

Kwa mujibu wa Mkuu wa kitengo cha Uhusiano MOI, Patrick Mvungi alisema mitambo imewasili bandari ya Dar es salaam na inatarajiwa kusimikwa MOI.

Ujio wa mitambo hiyo mipya na ya kisasa inayotoka Nchini Ujerumani, ni juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha Sekta ya Afya hapa nchini.

"Mitambo ya Maabara ya upasuaji wa Ubongo bila kufungua fuvu (Angio Suite) imewasili bandari ya Dar es salaam.Mitambo, Vifaa vingine pamoja na ukarabati wa Chumba vimegharamiwa na Serikali kwa gharama ya Tsh Bilioni 7.9." Alieleza Patrick Mvungi.

Na kuongeza kuwa ujio wa mitambo hiyo ya upasuaji wa ubongo bila kufungua fuvu itakuwa msaada mkubwa kwa wananchi na mataifa mengine hapa Barani Afrika.

"Taasisi ya Mifupa-MOI pia tunatoa huduma mbalimbali za kibingwa na kibobezi zikiwemo;Upasuaji wa Kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye Ubongo,Upasuaji wa Mgongo kwa kufungua eneo dogo.

Zipo pia huduma za Upasuaji wa magoti kwa njia ya matundu, Upasuaji wa kupandikiza nyonga bandia, Upasuaji wa kupandikiza goti bandia na Upasuaji wa kuondoa uvimbe kwenye ubongo alieleza Mkuu huyo wa kitengo cha Uhusiano MOI, Patrick Mvungi.

Kwa sasa huduma hizo na nyingine zinapatika nchini kufuatia maboresho katika sekta ya Afya ambapo awali zilikuwa zinapatikana nje ya Nchi kwa gharama kubwa.

Picha za mitambo ya Angio Suite muonekano wake.



Kontena zilizobeba mitambo hiyo ya Angio Suite zikiwa bandari ya Dar Es Salaam baada ya kuwasili kutoka Nchini Ujerunani. (Picha na kitengo cha Uhusiano MOI).

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages