Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo (wa pili kulia) akiwasili ofisi za
Wizara eneo la Mtumba jijini Dodoma jana
na kupokewa na viongozi pamoja na watumishi wa Wizara hiyo ikiwa ni mara yake
ya kwanza tangu ateuliwa katika nafasi hiyo.Wa tatu kulia ni Naibu Katibu Mkuu
Nicolaus Benjamin.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo akisalimiana na Mthamini Mkuu wa Serikali
Evalyne Mugasha alipowasili ofisi za Wizara
eneo la Mtumba jijini Dodoma jana ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu
ateuliwa katika nafasi hiyo.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara hiyo Mary Makondo alipowasili ofisi za
Wizara ya Ardhi eneo la Mtumba jijini
Dodoma jana ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu ateuliwa kushika nafasi hiyo.
Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mary Makondo (Hayupo pichani) alipowasili
ofisi za Wizara ya Ardhi eneo la Mtumba
jijini Dodoma jana ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu ateuliwa kushika nafasi
hiyo.(PICHA NA HASSAN MABUYE WIZARA YA
ARDHI)
Na Munir Shemweta, WANMM DODOMA
Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mary Makondo amewataka watumishi wa sekta
ya ardhi katika Wizara hiyo kushirikiana ili kuibadilisha Wizara na kuwa na
utendaji bora utakaokidhi mahitaji ya wananchi.
Makondo alisema hayo jana
wakati akizungumza na watumishi wa wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi alipowasili kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kushika wadhifa huo.
Makondo alichukua nafasi hiyo
kutoka kwa Dorothy Mwanyika aliyestaafu kwa mujibu wa Sheria. Kabla ya Uteuzi
huo Makondo alikuwa Kamishna wa Ardhi kwenye Wizara ya Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi.
Alisema, mategemeo ya
watumishi wa Wizara ya Ardhi mara baada ya kuteuliwa kwake ni makubwa lakini
msisitizo wake ni watumishi hao kufanya kazi kwa bidii na kwa kujituma ili
kuweza kuibadilisha Wizara.
‘’Kauli ya Wizara kuwa
ina ‘madudu’ siyo nzuri hivyo tukimbie ili tuwe na sekta ya ardhi
iliyobadilika’’ alisema Makondo.
Katibu Mkuu huyo wa
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alitaka kuthaminiwa kwa mchango
wa kila mtumishi wa Wizara hiyo kwa kuwa ndiyo njia pekee itakayoleta mabadiliko
na mafanikio ya utendaji kazi wa sekta hiyo.
Kwa mujibu wa Makondo,
Kampuni ya utengenezaji magari ya Toyota imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwenye
biashara zake kutokana na kutumia mfumo wa Kaizen unaothamini mchango wa kila mmoja
katika utendaji kazi.
Makondo amewataka pia
watumishi wa Wizara ya Ardhi kuweka miakakati ya pamoja kwa lengo la
kuibadilisha wizara hapo ilipo ili kuonesha kuwa wizara hiyo imebadilika katika
utendaji wake.
Baadhi ya Watumishi wa
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi walioneshwa kufurahishwa na
uteuzi wa Katibu Mkuu huyo kwa kuwa ametokea Wizara hiyo na anaijua sekta ya
ardhi vizuri pamoja na watumishi wake.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇