LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 16, 2020

JAJI WA MAHAKAMA KUU YA ZANZIBAR MKUSA ISSAC SEPETU AMEFARIKI DUNIA LEO

Na Happiness Katabazi
JAJI  Mkusa Issack Sepetu  ambaye amefariki Leo asubuhi Zanzibar alikuwa ni Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar na anatarajiwa kuzikwa leo saa kumi eneo la Mbuzini , Zanzibar.

Enzi za uhai wake marehemu aliteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , Kaimu Jaji Mkuu Zanzibar, Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama na Mwenyekiti wa Mahakama ya Kazi.

Jaji Mkusa mchango wake alioutoa katika tasnia ya sheria kupitia mashauri  mbalimbali alizozisikiliza na kuzitolea uamuzi utakumbukwa.

Pole Jaji Mkuu wa Zanzibar  Omar Othman  Makungu na watumishi wa mhimili wa mahakama Zanzibar , familia na ndugu na jamaa na marafiki kwa kuondokewa na mpendwa wenu Jaji Mkusa.

Sisi tulimpenda Jaji Mkusa ila Mungu kampenda zaidi.
16/2/2020.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages