LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 6, 2020

DK. BASHIRU AKABIDHI MSAADA WA MASHINE YA FOTOKOPI YA SH. MILIONI 1.5 KWA MSTAAFU WA CCM

Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akizungumza na Mzee Shabani Kanijo baada ya kumkabidhi mashine ya Fotokopi yenye thamani ya sh. milioni 1.5, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Picha na Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM)

CCM Lumumba, Dar es Salaam
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ally amekabidhi mashine ya photokopi yenye thamani ya sh. 1.5 kwa mzee Shabani Kanijo (73) ambaye ni mstaafu katika kitengo cha Tehama cha CCM ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 43 ya kuzaliwa kwa CCM

Mzee Kanijo alikuwa ni mtumishi wa CCM tangu mwaka 1965 na alistaafu mwaka 2004, ambapo baadae alianza kusumbuliwa na maradhi na shughuli zake nyingi za kujipatia kipato zikasismama kwa muda mrefu.
Mapema mwaka huu Mzee Shabani  alifika Ofisi ya Katibu  Mkuu kuomba msaada hasa unaohusiana na taaluma yake ili aweze kujimudu na kujiendesha baada ya afya yake kuanza kuimarika, ambapo ombi lake kubwa lilikuwa ni kupata mashine ya photokopi kwa ajili ya kufufua steshenari yake iliyokuwa imesimama uendeshaji kwa kipindi chote cha ugonjwa.
Kama ilivyo utaratibu wa Chama Cha Mapinduzi kuwa karibu na makundi mbalimbali ya watu wenye uhitaji hasa wazee, leo tarehe 05 Februari, 2020 Makao Makuu ya CCM,  Dkt. Bashiru amemkabidhi vifaa vyote vya steshenari  ambapo mzee huyo ameishukuru CCM na kueleza kuwa,
“Anaishukuru sana CCM kwa kuendelea kuwa karibu na wazee, lakini zaidi naipongeza kwa kufanya mambo ambayo wakati wote yalikuwa yakipigiwa kelele  na sasa hata wapinzania hawana ajenda  tena.”
Ameongeza  kwa kuuliza kuwa,’’ Hao wapinzania wanataka nini tena? Kama hata wao mambo waliokuwa wanayataka CCM chini ya Rais Magufuli  imeyafanya yote.”
Aidha Katibu Mkuu amesisitiza kuwa, ni vema vifaa hivyo ama msaada wowote unaotolewa na Chama utumike kwa malengo yaliotarajiwa na sio vinginevyo ili msaada huo uwe na tija na Chama kiendelee kusaidia wenghine zaidi kwa kadri ya uwezo na mahitaji ya wenye uhitaji.
Ikumbukwe kuwa, leo ni siku ya kuzaliwa kwa CCM ambapo Chama hiko kinatimiza miaka 43 tangu kuundwa kwake kutoka vyama vya ukombozi vya TANU na ASP terehe 05 Februari, 1977.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages