Na Jastin Cosmas, Kibondo
Mwenyekiti wa Chamam Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Kigoma Amantusi Nzamba amewataka viongozi wa CCM Wilayani Kibondo kufanya kazi ipasavyo ili kuweza kusimamia ilani ya uchaguzi ya CCM vizuri.
Hayo ameyasema katika maadhimisho ya miaka 43 ya Chama Cha Mapinduzi yaliyofanyika jana katika Wilaya ya Kibondo ambapo Mwenyekiti huyo alipata fursa ya kutembelea baadhi ya shule za sekondari wilayani hapa ikiwemo shule ya Sekondari Maragarasi na kushiriki shughuli za ujenzi wa vyumba vya madarasa
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauli ya Kibondo Ndugu Rutema alisema idadi ya wanafunzi wanaofaulu mtihani wa darasa la saba na kujiunga na kidato cha kwanza inazidi kuongezeka hivyo wananchi hawana budi kuchangia nguvu kazi na serikali kumalizia pale walipo ishia.
Nae Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma Kajoro Vyoholoka amesema CCM imekuwa na mafanikio makubwa hivyo wananchi hawana budi kuchagua kiongozi bora atakae tatua changamoto za wananchi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Your Ad Spot
Feb 6, 2020
Home
Unlabelled
VIONGOZI CCM KIBONDO WAHIMIZWA KUSIMAMIA ILANI YA CCM IPASWAVYO
VIONGOZI CCM KIBONDO WAHIMIZWA KUSIMAMIA ILANI YA CCM IPASWAVYO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
Zaidi ni kuendelea kutangaza mazuri yanayofanywa na serikali ya CCM na kutumia vema nafasi walionazo katika kuhakikisha tunazidi songambele maana hatuhitaji kukwama kwa lolote@Tuchape Nazi kiongozi wenzanguuu!
ReplyDeleteZaidi ni kuendelea kutangaza mazuri yanayofanywa na serikali ya CCM na kutumia vema nafasi walionazo katika kuhakikisha tunazidi songambele maana hatuhitaji kukwama kwa lolote@Tuchape kazi kiongozi wenzanguuu!
ReplyDelete