LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 6, 2020

UWT DAR ES SALAAM WAPANIA KUPAMBANA KATIKA KUGOMBEA UONGOZI BADALA YA KUNGOJA VITU MAALUM

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam Dorothy Kilave akizungumza wakati akifungua Kikao Cha Baraza Kuu la Jumuiya hiyo mkoa huo wa Dar es Salaam, kilichofanyika jana katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Ilala. Kushoto ni Katibu wa UWT mkoa wa Dar es SalaamGrace Haule na Kulia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Taifa ya CCM na Mkuu wa Idara ya Siasa na Habari ya vyombo vya habari vya CCM vinavyosimamiwa na Kampuni ya Uhuru Media (UMG) Angel Akilimali. KUONA PICHA KEMKEM ZA KIKAO HICHO, TAFADHALI>> BOFYA HAPA

NA BASHIR NKOROMO, ILALA
Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Dar es Salaam umepania kuingia kilingeni kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ili kuchaguliwa badala ya kusubiri nafasi za viti maalum ambapo wahimizwa kujitokeza kwa wingi kugombea katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Akizungumza katika kikao cha Baraza Kuu la UWT mkoa wa Dar es Salaam, kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Ilala, Mwenyekiti wa UWT mkoa huo, Dorothy Kilave amesema umefikia wakati sasa wanawake nao kuingia katika kinyang'anyiro cha uchaguzi kwa kuwa wapo wengi wenye uwezo wa kuongoza.

"Kinamama sasa ni lazima tujiamini, kwa hiyo kila mmoja wetu anayejiona kuwa anao uwezo wa kuongoza itakapofika wakati wa uchaguzi ajitokeze kuomba kugombea, tunataka tupate nafasi za kuchaguliwa halafu viti maalum ibaki kuwa ni nafasi ya ziada tu.

Tatatizo letu kubwa sisi kina mama ni kwamba tunapoona mwenzetu amejitokeza kugombea uongozi tunakuwa na kinyongo naye tukidhani akipata ataturingia, tabia hiyo tuiache, mwenzetu akijitokeza tuwe wa kwanza kumuunga mkono mpaka ashinde kwenye uchaguzi", alisema Kilave.

Aliwataka wanawake hasa wa mkoa wa Dar es Salaam, kujiandikisha kwa wingi wakati wa maboresho ya daftari la kudumu la wapigakura kisha kuhakikisha siku ya kupiga kura wanajitokeza kwa wingi, akisema watakapojitokeza CCM lazima itahinda kwa kuwa wao ni 'Jeshi kubwa'.

Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Kilave alisema wanao uhakika kuwa Rais Dk. Magufuli atashinda kwa kura nyingi za kishindo kwa kuwa amekwishaonyesha uwezo wake wa kuongoza nchi kwa kufanya mambo mengi ambayo Watanzania walikuwa na kiu yao.

"Kwa upande wa Urais hatuna wasiwasi, tunajua tunashinda kwa kishindo sasa kilichobaki kushikamane kuhakikisha tunashinda pia katika nafasi hizi nyingine za Ubunge na udiwani, na ninaamini tukiwa na mshikamano tutanyakua viti vyote hasa katika mkoa wetu huu wa Dar es Salaam", alisema Kilave.

Mapema, akitambulishwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Taifa ya CCM na Mkuu wa Idara ya Siasa na Habari ya vyombo vya habari vya CCM vinavyosimamiwa na Kampuni ya Uhuru Media (UMG) Angel Akilimali aliwataka Jumuiya ya UWT  kuwa karibu na vyombo vya habari vya CCM ili kupata habari za ukweli na uhakika zikiwemo zinazokihusu chama.

"Vyombo vyetu hivi vya Magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Uhuru FM na Channel ten, mkivitumia kila mara kutangaza matukio mbalimbali na kuwa mnasilikiza, kutazama na kusoma mtapata manufaa makubwa maana hivi sasa vimekuwa imara sana", aliseama Angel.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages