Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya watu wa Zanzibar PBZ Juma Ameir Hafidh
akitoa maelezo kuhusu huduma za uwakala katika hafla ya Uzinduzi wa
Huduma za PBZ wakala na Visa Card iliofanyika katika Uwanja wa Mnara wa
kumbukumbu wa miaka 50 ya Mapinduzi (MAPINDUZI SQUARE)Kisonge
Zanzibar.Ikiwa ni shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Khamis Mussa Omar akitoa maelezo
katika hafla ya Uzinduzi wa Huduma za PBZ wakala na Visa Card
iliofanyika katika Uwanja wa Mnara wa kumbukumbu wa miaka 50 ya
Mapinduzi (MAPINDUZI SQUARE)Kisonge Zanzibar.Ikiwa ni shamra shamra za
miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa
Haji Ussi Gavu akiweka kidole katika mashine ya kusajilia ikiwa ni
ishara ya Uzinduzi wa Huduma za PBZ wakala na Visa Card iliofanyika
katika Uwanja wa Mnara wa kumbukumbu wa miaka 50 ya Mapinduzi (MAPINDUZI
SQUARE)Kisonge Zanzibar.Ikiwa ni shamra shamra za miaka 56 ya Mapinduzi
ya Zanzibar.
Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa akitoa hotuba
ya makaribisho kwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Huduma za PBZ wakala
na Visa Card iliofanyika katika Uwanja wa Mnara wa kumbukumbu wa miaka
50 ya Mapinduzi (MAPINDUZI SQUARE)Kisonge Zanzibar.Ikiwa ni shamra
shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa
Haji Ussi Gavu(wapili kulia )akiabidhiwa Visa Card na Waziri wa Fedha na
Mipango Baloz Mohamed Ramia Abdiwawa katika Uzinduzi wa Huduma za PBZ
wakala na Visa Card iliofanyika katika Uwanja wa Mnara wa kumbukumbu wa
miaka 50 ya Mapinduzi (MAPINDUZI SQUARE)Kisonge Zanzibar.Ikiwa ni shamra
shamra za miaka 56 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Na Khadija Khamis Maelezo Zanzibar 02/01/2020.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Issa Haji Ussi Gavu amesema huduma za PBZ Wakala zitasaidia kuimarisha utendaji wa kazi katika kutoa huduma za Wateja .
Hayo aliyasema wakati wa uzinduzi wa huduma za Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) wakala iliofanyika katika kiwanja cha Mapinduzi Square.Kisonge .
Alisema kuimarishwa huduma za kibenki katika mifumo mbali mbali ya kuimarisha huduma hizo kutawasaidia wateja kutafuta huduma kwa masafa marefu pamoja na kupunguza msongamano wa wateja katika benki hizo .
Aidha alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya awamu ya saba katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wananchi katika sekta mbali mbali kwa kuanzishwa mfumo madhubuti ya mitandao ya kijamii katika sehemu tofauti na kuwawekea wakala katika kila wilaya pamoja na viza ili kuwaondoshea usumbuvu wateja wao .
Waziri Gavu alisema kukamilika kwa mfumo wa kutoa huduma kwa njia ya wakala pamoja na viza kutatoa nafasi kwa wateja kupata uhakika wa kutoa pesa zao .
Akitoa wito kwa wakala hao aliwataka watoe ushirikiano kwa wateja pamoja na kujenga heshima na uwaminifu jambo ambalo litaijengea hadhi benki hiyo ili kufikia lengo lililokusudiwa.
Nae Waziri wa Fedha na Mipango Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa alisema huduma za kibenki kwa upande wa Zanzibar zilianza miaka miwili tu baada ya Mapinduzi kwa lengo la kuwaletea maendeleo ya watu wa Zanzibar .
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Khamis Mussa amesema maendeleo katika nchi yanategemea ukuwaji wa mageuzi ya kiuchumi .
Alisema ongezeko la ukuwaji wa uchumi umeongezeka kwa kasi kubwa tofauti na kabla ya Mapinduzi ilivyokuwa .
Alifahamisha kuwa benki 13 zinazotoa huduma hapa Zanzibar ni ishara ya ukuwaji wa uchumi ambao unakwenda sambamba na uwekaji wa amana na mikopo kwa wateja wa benki .
Alisema uzinduzi wa huduma za Benki ya Watu wa Zanzibar Wakala na viza ni hatua muhimu ya kuimarisha maedeleo ya kiuchumi kwa watu wa Zanzibar.
Mapema Mkurugenzi Mtendaji Juma Ameir Hafidhi amesema kukamilika kwa mfumo wa kisasa wa malipo ya mitandao ya kijamii kutatoa fursa ya kupata huduma kwa njia ya simu ya mkononi kwa kupata huduma za kibenki pamoja na mitandao ya kijamii.
Alifahamisha kuwa mfumo huu utarahisishwa kufanya malipo kwa mitandao ya kijamii kufanya biashara pamoja na malipo kwa kutumia kadi.
Hata hivyo alisema mfumo huo itasaidia kuimarisha mtandao wa kimataifa na sehemu mbali mbali zinazotoa huduma hizo kwa wateja ikiwemo kulipia kwa kupata huduma mbali mbali .
Huduma za kibenki zilianziswa Zanzibar katika mwaka 1966 hadi sasa zinatimiza miaka 54 ni miaka miwili kabla ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar .

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇