Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini,
Prof. Sospeter Muhongo amepanga kuongoza
harambee ya kuchangia fedha za kujengea vyumba vya madarasa 13 katika
shule zenye ufungufu jimboni humo.
Katika harambee hiyo Prof. Muhongo
atawashirikisha wanavijiji mbalimbali ili kutimiza lengo la kunusuru hali hiyo
itakayookoa wanafunzi 616 wanaotarajia kujiunga Kidato cha Kwanza mwaka huu
katika shule hizo zenye upungufu wa vyumva vya madarasa.
Mbunge Muhongo anataajia kutembelea
shule zote za sekondari zenye upungufu huo na hatimaye kuandaa harambee ya
kuwezesha ujenzi wa vyumba hivyo haraka iwezekanavyo ili wanafunzi wasikose
kujiunga.
“Shule zinafunguliwa Jumatatu, tarehe
6.1.2020, bado tunao upungufu wa vyumba 13 vya Madarasa ya Kidato cha Kwanza
(Form I).
Vyumba 13 hivyo visipopatikana wanafunzi
616 watabaki nyumbani wakisubiri uwepo wa Vyumba vya Madarasa yao,”
alisema Prof. Muhongo hivi karibuni jimboni humo.
.
Ameanza kutembelea shule hizo leo na
kuona kila shule vyumba vilivyopungua.
Ratiba kamili ya kukagua shule hizo
ni kama ifuatavyo; upungufu wa vyumba kwenye mabano.
Tarehe 2.1.2020
Saa 4 Asubuhi
Busambara Secondary School (Mpya)
Saa 8 Mchana
Bugwema Sekondary School (Vyumba 3)
Tarehe 3.1.2020
Saa 4 Asubuhi
Dan Mapigano Memorial Secondary
School (Mpya)
Saa 8 Mchana
Bulinga Secondary School (Vyumba 3)
Tarehe 6.1.2020
Saa 4 Asubuhi
Nyakatende Secondary School (Vyumba
2)
Saa 8 Mchana
Rusoli Secondary School (Chumba 1)
Kasoma Secondary School (Vyumba 3)
na Nyanja Secondary School (Chumba 1) BADO WANAJIPANGA
Kwa WANAOPENDA KUCHANGIA ujenzi huo
hata kwa kupitia Akaunti za Benki za Sekondari hizo, wanaombwa wapewe
mawasiliano ya KUCHANGIA kutoka kwa:
Fedson: 0765 59 28 28
Hamisa: 0762 62 68 81
Verediana: 0764 23 98 21
SISI SOTE tunaombwa TUCHANGIE UJENZI
WA VYUMBA 13 vinavyohitajika ili WANAFUNZI 619 wa FORM I wa Jimboni mwetu
WASIKOSE kuanza MASOMO yao ya Sekondari.
HERI YA MWAKA MPYA WENYE MAFANIKIO
MAKUBWA
TUHAKIKISHE
WANAFUNZI WALIOFAULU NA KUCHAGULIWA KUJIUNGA NA FORM I JANUARI 2020 WANAENDA
KUANZA MASOMO YAO KWENYE SEKONDARI WALIZOPANGIWA
KIDATO
CHA KWANZA 2020 - KIMEPUNGUKIWA VYUMBA VYA MADARASA 13, WANAFUNZI 619 WATABAKI
NYUMBANI
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇