Wiki iliyopita, tarehe 28 Desemba 2019 nilitimiza miaka
70 tangu kuzaliwa. Kwangu kufikia umri huo ni kwa kudra na rehema za
Mwenyezi Mungu. Hivyo basi tulikuwa na Ibada ya shukrani hapo kijijini
Lufilyo, Busokelo iliyoongozwa na Baba Askofu Ambele Mwaipopo wa Kanisa
la Kiinjili la Kiluteri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Ziwa Tanganyika na
Baba Askofu Panja wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la kusini,
wakisaidiwa na Baba Mchungaji Mwasanguti wa KKKT Dayosisi ya Konde,
Jimbo la Kati.
Ibada
ilihudhuriwa na wananchi na wageni waalikwa kutoka Rungwe, Busokelo,
Kyela, Dar es Salaam, Arusha Singida na Kigoma, na Waheshimiwa Madiwani
wa Halmashauri za Wilaya za Rungwe na Busokelo.
Walikuwepo
pia wageni kutoka Kenya, Uganda, Zambia, Malawi, Uingereza na Ujerumani
na baadhi ya Walimu walimfundisha Prof. Mark Mwandosya Shule ya
Sekondari ya Malangali zaidi ya miaka 50 iliyopita.
Pichani kutoka kulia ni wafuatao:Mhe.
Balozi Chirau Ali Mwakwere, aliyekuwa Balozi wa Kenya nchini na Waziri
wa zamani wa Mambo ya Nje wa Kenya; Baba Mchungaji Mwasanguti; Mwalimu
Charles Muhitira aliyenifundisha Historia na Hisabati kidato cha kwanza
na cha pili; Mwalinu Clement Bendera aliyenifundisha Kemia, Fizikia na
Jiografia kidato cha tatu na cha nne; Baba Askofu Ambele Mwaipopo wa
KKKT Dayosisi ya Ziwa Tanganyika; Mwalimu Ambangile Mwakilembe
aliyenifundisha Kiswahili kidato cha nne; Mimi; Mama Lucy Mwandosya; na
Baba Askofu Panja wa Kanisa la Moravian, Jimbo la Kusini.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇