Hii ni baada ya Rais Nkurunziza kutoa msamaha kwa wafungwa waliohukumiwa vifungo visivyozidi miaka mitano jela pamoja na wafungwa wajawazito, akina mama wanaonyonyesha na walemavu.
Hatua hiyo imetajwa kuwa itakayosaidia kupunguza msongamano wa sasa katika jela zote za Burundi. Taarifa zinasema kuwa, jela kuu ya Mbimba ya mjini Bujumbura, ilijengwa ikiwa na uwezo wa kuwahifadhi wafungwa 800 pekee, lakini kwa sasa lina zaidi ya wafungwa 4000.
Jiunge na mwandishi wetu wa mjini Bujumbura, Hamida Issa kwa kubonyeza alama ya sauti pale juu………………./
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇