Wanafunzi, Walimu, Wazazi, Viongozi wa Serikali na Chama
(CCM) wamehudhuria SHEREHE za UZINDUZI wa AGAPE Primary School
zilizofanyila Jumanne, 7.1.2020 Kijijini Bukima.
KIONGOZI na MMLIKI wa Shule hiyo, Ndugu ANDREW KAYOLE
(32yr), mhitimu wa UDOM, Shahada ya Biashara Bc(HRM) amesema Shule hiyo
ilisajiliwa rasmi tarehe 21.6.2017 na tayari WAHITIMU wa kwanza
wamemaliza Darasa la 7 (Std 7) Mwaka jana (2019) wakiwa wa KWANZA kwa
Wilaya ya Musoma katika kundi lao.
Wanafunzi wote walifaulu (A&B).
Shule inafundisha kwa lugha ya KIINGEREZA na Mwakani lugha ya KIFARANSA
itaanza kufundishwa Shuleni hapo.
MGENI RASMI, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof
Sospeter Muhongo amesema kwamba kuwepo kwa Shule Binafsi (Private
Schools) Jimboni mwao ni muhimu sana kwa UIMARIKAJI wa UBORA wa ELIMU
kupitia USHINDANI KITAALUMA kwa Shule zote za Msingi zilizoko Jimboni
humo (Shule 3 za Binafsi na 111 za Serikali).
Mbunge huyo amekuwa AKICHANGIA MAENDELEO ya Shule za
Msingi na Sekondari za Serikali na Binafsi bila UBAGUZI wo wote.
Aliwakumbusha WAGENI waalikwa kwamba Vyuo Vikuu bora Duniani vimo vya
Binafsi (Private Universities) kama vile Harvard (USA), MIT (USA), Yale
(USA) Caltech (USA), na vilevile vimo vya umma (Public Universities)
kama vile Oxford (UK) na Cambridge (UK).
Mbunge huyo amechangia box 10 za VITABU vya Maktaba
ya Shule hiyo. Vilevile, amechangia SARUJI MIFUKO 50 kwa ajili ya
ujenzi wa Jengo la TEHAMA. Ametoa ahadi ya kuchangia COMPUTER 1 na
PRINTER 1 mara Jengo hilo litakapokamilika na kuanza kutumika.
Wakati akizindua AGAPE Primary School na kuweka Jiwe la
Msingi la Jengo la TEHAMA la Shule hiyo, Mbunge huyo AMEMWOMBA
MWANZILISHI wa Shule hiyo aendelee kuipanua hadi kuanza kutoa MASOMO ya
SEKONDARI.
WAZALIWA KUWEKEZA VIJIJINI MWAO
MMILIKI (Ndugu ANDREW KAYOLE) wa Agape Primary School ni
KIJANA (32yr) ALIYETHUBUTU na KUFANIKIWA kuwekeza Kijiji mwao.
Mbunge
wa Jimbo AMEMPONGEZA SANA na kusema JIMBO LINAJIVUNIA kuwa na WAWEKEZAJI
wa aina hiyo – TUJIFUNZE KWAKE na TUWEKEZE Vijijini kwetu!
Profesa Muhongo akiangalia jiwe la msingi baada ya kuizindua rasmi shule hiyo.
Profesa Muhongo akiwa na viongozi wengine pamoja baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Muhongo (kulia) akizungumza jambo na viongozi pamoja na mmiliki wa shule hiyo, Kayole.
Prof. MUHONGO AKIWA NA BAADHI YA VIONGOZI PAMOJA NA BAADHI YA WANAFUNZI BAADA YA KUZINDUA SHULE HIYO YA AGAPE.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇