Mtunukiwa wa Tuzo ya Heshima ya
Udaktari (PhD) Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Horticultural
Association (TAHA), Dkt. Jaquelin Mkindi, akiwa katika mahafali ya 39 ya
Chuo cha Africa Graduate University yaliyofanyika jijini Arusha hivi
karibuni.Mtunukiwa
wa Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD) Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania
Horticultural Association (TAHA), Dkt. Jaquelin Mkindi, akihutubia
baada ya kutunukiwa tuzo hiyo. Mtunukiwa
wa Tuzo ya Heshima ya Udaktari (PhD) Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania
Horticultural Association (TAHA), Dkt. Jaquelin Mkindi, akiingia
ukumbini.
Mtunukiwa wa Tuzo ya Heshima ya
Udaktari (PhD) Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Horticultural
Association (TAHA), Dkt. Jaquelin Mkindi (wa tatu kulia waliokaa) akiwa
katika picha ya pamoja na mgeni rasmi na waalikwa wengine baada ya
kutunukiwa tuzo hiyo.
………………………………………….
Na Dotto Mwaibale
CHUO cha Africa Graduate
University Kampasi ya Uingereza kimemtunuku Tuzo ya Heshima ya Udaktari
(PhD) Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Horticultural Association (TAHA),
Dkt. Jaquelin Mkindi.
Waliotunukiwa tuzo hizo za
heshima ni wale waliotoa mchango mkubwa kwa kufanya shughuli mbalimbali
za kujitolea za kijamii na zikaleta manufaa kwa mtu mmoja mmoja na taifa
kwa ujumla.
Akizungumza wakati wa mahafali ya
39 ya chuo hicho, Makamu Mkuu wa Chuo hicho chenye makao makuu yake
nchini Sierra Leone, Profesa Timothy Kazembe, alisema kila mwaka
kimekuwa kikitoa Tuzo za heshima na Shahada za Uzamili kwa watanzania
waliotoa mchango wa kusaidia jamii katika shughuli mbalimbali.
“Tunao watunuku tuzo hizi tuzo za
heshima ni watu waliokuwa na umri wa miaka 60 ambao wanafanya kazi za
kijamii katika nyumba za ibada kwa zaidi ya miaka 15 na kuendelea
na wale ambao umri wao ni miaka 40 hadi zaidi na wenye shahada” alisema
Profesa Kazembe.
Mkindi ametunukiwa Tuzo hiyo
kutokana na mchango wake mkubwa katika jamii kwani ndiye mwanzilishi wa
Taasisi isiyo ya kiserikali ambayo inafanya vizuri katika masuala ya
kilimo hapa nchini.
Katika mahafali hayo
yaliyofanyika Hoteli ya Gran Melia jijini Arusha na kupambwa na Bendi ya
Jeshi la Polisi kutoka Chuo cha Polisi (CCP) yalihudhuriwa na watu
maarufu na mgeni rasmi alikuwa ni Makamu Mkuu wa Chuo cha Nelson Mandela
African Institute of Science and Technology, Profesa Emmanuel Luoga
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇