Askofu
wa Jimbo Katoliki Singida, Mhashamu Edward Mapunda, akipanda kwenye
sehemu ya juu ya Kituo cha Hija Sukamahela kwa ajili ya kutoa baraka
kabla ya misa takatifu. Kituo hicho kimejengwa eneo la Sukamahela,
wilaya ya Manyoni mkoani Singida eneo ambalo lipo katikati ya Tanzania.
Mwonekano
wa Kituo kipya cha hija cha sukamahela, kilichojengwa kwa heshima ya
Bikira Maria na kuzinduliwa ( juzi) eneo la Sukamahela, wilaya ya
Manyoni mkoani Singida.
Waumini wakipanda juu ya mwinuko wa eneo kilipojengwa kituo hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akihutubia.
Msafara kwa ajili ya uzinduzi.
Shughuli ya uzinduzi ikiendelea.
Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akipata upako wa maji ya Baraka
kutoka kwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Singida, Mhashamu Edward Mapunda.
Na Mwandishi Wetu, Singida
KAULI
ya kwamba Singida ni njema tena ni njema sana, imezidi kujidhihirisha
baada ya mkoa huo kubarikiwa kuanza mwaka wa 2020 kwa tukio la aina yake
la uzinduzi wa kituo cha hija kwa heshima ya Bikira Maria kilichopo
eneo la Sukamahela, mahali ambapo ni katikati ya nchi ya Tanzania,
wilaya ya Manyoni mkoani hapa
Kituo
cha Sukamahela ambacho watu watakuwa wakikusanyika kila ifikapo Desemba
9, na ambacho kimejengwa kwa ustadi mkubwa kinakuwa ni cha pili ndani
ya mkoa wa Singida, kikitanguliwa na kile cha kwanza kilichopo eneo la
Kimbwi nje kidogo ya mji, ambacho pia kwa lengo lile lile hutoa fursa ya
watu kukutana na Mungu kwa njia ya Bikira Maria ifikapo Septemba kila
mwaka
Akizindua
Kituo hicho juzi, Askofu wa Jimbo Katoliki la Singida, Mhashamu Edward
Mapunda, alisema kituo cha hija Sukamahela kinakwenda kutoa fursa ya
watu kujikabidhi kwa mama Bikira Maria msaada wa daima kwa maombezi
“Kituo
hiki hakikuzinduliwa kwa bahati mbaya ni zawadi ya Mwenyezi Mungu kwa
binadamu wote. Na tusisubiri hadi tarehe 9 Desemba pekee ndio
tukusanyike hapa bali kila mara tukipata nafasi tufike…kila anayepita
eneo hili asiache kuchepuka hapa au usisahau kupiga ishara ya msalaba
ukimwambia mama napita hapa,” alisema Mapunda
Alisema
kwa kuzingatia kwamba binadamu wote wanakwenda kwa Yesu Kristu kupitia
Bikira Maria ni dhahiri uwepo wa kituo hicho utasaidia sana kuimarisha
imani na kuleta chachu ya uinjilishaji, pia ni fursa ya Baraka na neema
katika kuombea amani ya familia, mkoa na taifa, sambamba na kuimarisha
ibada za waumini kupitia mama huyo
Hata
hivyo, Askofu Mapunda kwa namna ya pekee alimshukuru na kumpongeza Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Dk Rehema Nchimbi, ambaye mbali ya kuwa rafiki
mzuri wa Bikira Maria lakini pia ndiye mwasisi wa wazo hilo takatifu kwa
kuona na hatimaye kushauri jumuiya ya kanisa hilo kujenga kituo cha
hija mahali hapo
“Tunamshukuru
sana Mkuu wa Mkoa mama Nchimbi, wazo hili limetoka kwa Mungu kupitia
yeye. Siku aliponiletea wazo hili na nilipotafakari nikaona ni wazo la
Mungu na ni ufunuo, maana mambo haya ni ya kimungu na Mwenyezi Mungu
anaweza kumfunulia yeyote…na hatimaye tulilipokea kwa mikono miwili,”
alisema Askofu wa Jimbo Katoliki la Singida
Aidha,
Mapunda kupitia Mkuu wa Mkoa, alimshukuru Rais John Magufuli kwa
mchango wake katika kufanikisha ujenzi wa kituo hicho cha hija, alioutoa
hivi karibuni akiwa safarini wakati alipopita mkoani hapa kuelekea
chato mkoani Geita kwa mapumziko
Akiwasilisha
ujumbe wa siku ya amani kwa mwaka mpya 2020 kutoka kwa Kiongozi wa
Kanisa Katoliki duniani, Papa Francisco, Askofu Mapunda alisema amani ni
safari ya matumaini, majadiliano, upatanisho, uongofu wa ekolojia
(mazingira) na haiwezi kujengeka kwa vitisho na hofu ya maangamizi
“Amani
ya kweli inafumbatwa katika mifumo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi
inayozingatia haki na msamaha, hivyo tujitahidi kila mmoja wetu kuwa
chombo cha amani,” alisema Askofu Mapunda akimnukuu Papa Francisco
Zaidi,
wakati taifa likielekea kwenye uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na
Madiwani utakaofanyika mwaka huu, Askofu Mapunda aliwasihi watanzania
kote nchini kuiweka nchi katika sala, hasa kupitia Bikira Maria ili
aweke uchaguzi huo kwenye moyo wake mtakatifu, kwasababu yeye ni ‘Malkia
wa Amani’
Kwa
upande wake mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Nchimbi, alisema kila
Mtanzania anapaswa kuwa shahidi juu ya ushuhuda wa wazi usio na mashaka
kuhusu upendo mkubwa na uwajibikaji wa Bikira Maria kwa ulinzi wake,
malezi, maombezi na usalama wa Taifa.
Alisema
anakumbuka jinsi uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2015 ulivyojaa
misukosuko, hofu na mashaka, wasiwasi na hata wengine walitamani
kuikimbia Tanzania, huku akikiri kwamba kilichotuvusha salama sio
kingine bali ni Bikira Maria
“Ndio
maana mama huyu hatimaye leo hii amesimama katikati ya nchi hii hapa
Sukamahela ili kuendelea kutuvusha. Tusichoke kumkimbilia, tusichoke
kumuomba amani ya taifa letu kupitia sala na maombezi yake”. Alisema
Nchimbi
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇