LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 5, 2020

HARAMBEE ILIYOENDESHWA NA PROFESA MUHONGO YA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA, VYOO YAFANIKIWA MUSOMA VIJIJINI, YAWAOKOA WANAFUNZI KUKOSA KIDATO CHA KWANZA


Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo (mwenye T-shirt ya bluu) akiwa na Wananchi wa Kata ya Busambara wakati wa kikao cha harambee ya kuchangia ujenzi wa vyoo vya Busambara Secondary School.


 Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Muhongo (mwenye T-shirt ya bluu) akiwana baadhi ya wananchi wakati wa harambee.

Ujenzi wa Jengo la  Vyoo ukiendelea juzi
 Wananchi wa Kata ya Bugoji wakipiga HARAMBEE ya kukamilisha ujenzi wa vyoo vya Dan Mapigano Memorial Secondary School.Harambee hiyo ilisimamiwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Prof. Muhongo.


 Na Mwandishi Wetu, Musoma Vijijini

Mbunge wa Jimbo Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo amefanya vikao vya harambee na wazaliwa wa Kata zenye upungufu wa vyumba vya madarasa ili kupata fedha za kukamilisha ujenzi wa vyumba vipya vinavyohitajika kwenye Sekondari  jimboni humo.

Baadhi ya wakazi wa maeneo hayo wamejitokeza kuchangia ujenzi huo, huku wakiongezwa nguvu na Mbunge wao ili kukamilisha ujenzi huo kwa muda unaotakiwa, kwa lengo la kuhakikisha  hakuna mwanafunzi atakayebaki nyumbani.

 Michango hiyo itasaidia wanafunzi 3,480 wa Sekondari za Kata  na za Bweni waliochaguliwa jimboni humo, kuendelea na masomo baada ya vyumba vya madarasa kujengwa.

“Hakuna  mwanafunzi atakayebaki nyumbani kwa sababu ya ukosefu  wa vyumba vya madarasa. Muhimu ni kupatikana kwa vyumba vipya ili kila darasa lichukue Wanafunzi wasiozidi 40,” alisema Profesa Muhongo.

SEKONDARI   2 MPYA ZINAZOJENGWA JIMBONI ZAOMBA ZIFUNGULIWE TAREHE 13.1.2020

(1) Busambara Secondary School  ya Kata ya Busambara (Vijiji vya Maneke, Kwikuba na Mwiringo). 

Vyumba vipya 3 vya Madarasa na madawati 40 kila darasa viko tayari. Jengo la Ofisi za Walimu linakamilishwa kwa kuwekwa milango na madirisha. Ujenzi wa Vyoo vya Wasichana, Wavulana na Walimu utakamilika Alhamisi, 9.1.2020.

Kikao  cha harambee cha wananchi na Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo, cha tarehe 2.1.2020 kimetoa msukumo mkubwa wa ukamilishaji wa ujenzi huo. 

Mbali ya  michango ya awali ya Mbunge huyo, amekubali pia kununa rangi ya kupaka ndani na nje ya majengo hayo matatu  ya Vyoo na Jengo la Ofisi za Walimu. Baadhi ya  Wazaliwa  Kata ya Busambara  wanaendelea kuchangia  ujenzi wa Sekondari ya Kata yao - AHSANTENI SANA!

Wananchi wa Vijiji 3 vya Kata ya Busambara wameandika barua wakiiomba Serikali iwaruhusu Sekondari yao ifunguliwe  tarehe 13.1.2020 na kuchukua Wanafunzi 142 ya Kata yao waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza Januari 2020. 

(2) Dan Mapigano Memorial Secondary School ya Kata ya Bugoji (Vijiji vya Kanderema, Kaburabura na Bugoji)

Vyumba vipya 5 vya Madarasa na madawati 40 ya kila darasa viko tayari. Ofisi za Walimu zimekamilika. Ujenzi wa vyoo  vyote (wasichana, wavulana na walimu) vya shule utakamilika ifikapo Jumatano, 8.1.2020. Kwenye HARAMBEE ya ujenzi huu, Mbunge wao, mbali ya MICHANGO yake ya awali, amechangia tena utengenezaji wa MILANGO mipya 12 ya Vyoo hivyo. Baadhi ya WAZALIWA wa Kata ya Bugoji wamechangia ujenzi wa Sekondari ya Kata yao.

Vijiji 3 vya Kata ya Bugoji vimeiiomba Serikali iwaruhusu Sekondari yao ifunguliwe tarehe 13.1.2020 na KUCHUKUA WANAFUNZI 141 wa Kata hiyo waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza Januari 2020.

KUPUNGUZA MRUNDIKANO WA WANAFUNZI MADARASANI

Vyumba VIPYA vya Madarasa VIZIPOPATIKANA kwenye baadhi ya Sekondari patakuwepo na MRUNDIKANO MKUBWA wa Wanafunzi madarasani mwao:
Bugwema (vyumba vipya 3 vinahitajika), Bulinga (3), Kasoma (3), Nyakatende (2), Nyanja (1) na Rusoli (1).

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages