Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na
Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na wajumbe wa kamati ya
maandilizi ya Sherehe ya Uhuru zitakazofanyika Kitaifa Mkoa wa Mwanza
wakiwasili kwa ajili ya Ukaguzi wa Uwanja wa CCM Kilumba utakaotumika
kwa ajili ya sherehe hizo.Alitembelea tarehe 30 Novemba 2019.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na
Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Afisa Maadhimishi
kutoka ofisi yake, Bw.Stephen Magoha alipowasili katika Kijiji cha
Hunghumalwa Wilayani Kwimba Mkoani Mwanza ili kukagua jeshi la jadi
(sungusungu) walioandaliwa kwa ajili ya kufanya onesho lao wakati wa
kilele cha sherehe za Uhuru (9 Desemba, 2019).
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na
Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiteta jambo na Mkuu wa itifaki
Balozi Kanali Wilbert Ibuge wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Kwimba
apotembelea kukagua maandalizi ya Jeshi la Jadi (Sungusungu)
wanaoendelea na maandalizi ya onesho maalumu katika sherehe za Uhuru
mwaka huu.
Mkuu wa
Itifaki Balozi Kanali Wilbert Ibuge akizungumza na Jeshi la Jadi (hawapo
pichani) wanaoendelea na maandalizi ya onesho maalumu katika sherehe za
Uhuru mwaka huu mkoani Mwanza.
Mkuu wa
Wilaya ya Kwimba Mhe. Senyi Ngaga na Mtemi wa Sungusungu wa Wilaya hiyo
Bw. Mogan Shimbi wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama wakati wa ziara yake kukagua maandalizi ya onesho maalum
la sungusungu katika wilaya hiyo.
Sehemu ya
wajumbe walioshiriki kukagua onesho la sungusungu Wilaya ya Kwimba
(hawapo pichani) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maadhimishi ya miaka
58 ya Uhuru kwa mwaka 2019.
Baadhi ya
wajumbe wa Jeshi la Jadi (sungusungu) wakiimba mbele ya Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye
Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na viongozi alioambatana nao
wakati wa ukaguzi wa maandalizi ya Maadhimishi ya 9 Desemba, 2019 mkoani
Mwanza.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na
Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Katibu Tawala wa Mkoa wa
Mwanza, Christopher Derek wakiangalia Gwaride la vikosi vya ulinzi na
usalama nchini ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Sherehe Uhuru kwa mwaka
2019.
Mtemi wa
Sungusungu wa Wilaya Kwimba mkoani Mwanza Bw.Mogan Shimbi akiwaongoza
wajumbe wa jeshi hilo kuimba wimbo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya
onesho lao la Maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru na miaka 57 ya Jamhuri.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
****************************************
NA.MWANDISHI WETU
Maandalizi
ya maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru yamefikia hatua za kuridhisha huku
Serikali ikieleza kuwa sherehe hiyo itapambwa na onesho maalum la Jeshi
la Jadi la sungusungu kutoka Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Uratibu, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameeleza itakuwa ni
mara ya kwanza kwa jeshi hilo kuonesha namna wanavyofanya kazi za ulinzi
katika maeneo yao ili kuendelea kuenzi nia ya Rais wa Awamu ya Tano
Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli ya kuilinda amani na utulivu uliopo nchini.
Waziri
alieleza hayo mapema Novemba 30, 2019 alipotembelea na kukagua
maandalzii ya onesho hilo yanayoendelea katika Kijiji cha Hunghumalwa
Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
“Hii
itakuwa ni mara ya kwanza kuwa na onesho hili maalum ambalo
linatukumbusha nia ya Mhe. Rais ya kuilinda amani iliyopo na kuhakikisha
haichezewi kwa gharama yoyote na kuona namna tunavyojivunia jeshi hili
lililoundwa katika misingi na maadili mema ya amani na utulivu,” alisema
waziri Mhagama
Aliongezea
kuwa, Jeshi hilo litajumuisha zaidi ya sungusungu 1300 watakaoshiriki
kwa siku hiyo kwa kuongozwa na Manji wao pamoja na Mtemi wa Wilaya Mogan
Shimbi.
Sambamba
na hilo maandalizi mengine ikiwemo, uandaaji wa uwanja wa CCM Kilumba,
mazoezi ya Majeshi (Gwaride), Usafi wa mazingira pamoja na vikundi vya
burudani yanaendelea mkoani hapo.
“Maandalizi
muhimu ikiwa ni pamoja na marekebisho ya miundombinu katika uwanja
yanaendelea pamoja na maandalizi muhimu ikiwemo, kutoa mialiko, kuandaa
malazi kwa wageni, kuandaa vikundi vya ngoma za asili, kuandaa gwaride ,
kuandaa wanafunzi wa watakaoumba umbo la bendera, pamoja na nyimbo za
kizazi kipya na mahitaji mengine muhimu yapo katika hatua za
kuridhisha,” alisema Waziri Mhagama
Aidha,
kutakuwa na vikundi vya burudani ikiwemo; ngoma za asili kutoka mkoa wa
Mara (Ritungu) na mkoa wa Mwanza, wimbo maalum kutoka Zanzibar pamoja na
kwaya ya AIC Mwanza na bendi ya Tanzania One Theatre (T.O.T)
vitatumbuiza.
Alifafanua
kuwa maonyesho hayo yatakayofanyika Desemba 9 yatajumuisha gwaride
maalumu la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama
nchini.
“Watoto
3200 kutoka shule za msingi na sekondari za mkoa wa Mwanza wataonesha
umbo la bendera ya Taifa letu,” alisema Waziri Mhagama
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella aliwasihi
Watanzania kumuunga mkono Rais Magufuli kwa kuendelea kuilinda amani
iliyopo kwa kuzingatia kaulimbiu ya mwaka huu pamoja na kuendelea kuwa
na uzalendo na kufanya kazi kwa bidiii kwa ajili ya kujiletea maendeleo.
Pia,
aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho hayo na
kuendelea kujiandaa kwa bidii, usanifu na ubunifu wa kipekee katika
kuiadhimisha siku hiyo muhimu.
“Ninamshukuru
sana Mhe. Rais kwa kuelekeza maadhimisho haya kufanyika mkoani kwetu,
niiwaase wananchi wa Mwanza kuitumia heshima tuliyopewa kwa kujitokeza
kwa wingi katika siku hiyo ili kuunga mkono jituhada za Mhe. Rais wetu,”
Alisisitiza Mongella.
Sherehe
za Maadhimisho ya Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri kwa mwaka huu
(2019) kitaifa yatafanyika Mkoani Mwanza katika viwanja vya CCM Kilumba
ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli na kupambwa na kauli mbiu
inayosema “Miaka 58 ya Uhuru na Miaka 57 ya Jamhuri; Uzalendo,
Uwajibikaji na Ubunifu ni msingi wa Ujenzi wa Uchumi wa Tifa letu”.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇