LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 12, 2019

WATU 275 WAMEUAWA NA BOKO HARAM

Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limetangaza kuwa, kwa akali watu 275 wameuawa na kundi la Boko Haram nchini Cameron tangu Januari mwaka huu.
Ripoti ya Amnesty International iliyotolewa jana Jumatano imeeleza kuwa, uchunguzi uliofanyika kwa majuma mawili unaonyesha kuwa, kwa uchache watu 275 wameuawa na wanamgambo wa Boko Haram huko nchini Cameron baina ya mwezi Januari na Novemba mwaka huu.
Kadhalika ripoti hiyo imeeleza jinsi raia wanavyotekwa nyara na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Boko Haram wanapofanya mashambulio yao katika maeneo mbalimbali ya Cameroon.
Samira Daoud, Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Amnesty International Katika Ukanda wa Magharibi na Katikati mwa Afrika anasema kuwa, watu wamekuwa wakiishi katika hofu na woga mkubwa na kwamba, wanahisi kuwa wametelekezwa bila msaada.
Rais Paul Biya wa Cameroon
Afisa huyo amesema kuwa, moja ya changamoto kubwa katika vita dhidi ya Boko Haram ni kuwa wanachama wa kundi hilo wanaishi msituni ilhali wanajeshi wanaoendesha vita dhidi ya wanamgambo hao wanaishi mjini.
Wafanyakazi wa mashirika ya misaada ya kibinadamu wanasema kuwa, mashambulio ya kigaidi yalianza tena nchini Cameroon baada ya Rais wa nchi hiyo Paul Biya kutangaza Januari mwaka huu kwamba, Boko Haram siyo tishio tena kwani wanachama wa kundi hilo wamefurushwa na kukimbilia nje ya mipaka ya nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages