Umati mkubwa wa wananchi wa Algeria jana walikusanyika katikati mwa mji mkuu wa nchi hiyo Algiers wakitaka kusitishwa uchaguzi wa Rais uliopangwa kufanyika leo Alhamisi. Waandamanaji hao walikuwa wakipiga nara hawatapiga kura leo katika uchaguzi huo wa Rais walioutaja kama mchezo wa kimaonyesho.
Wafanya maandamano nchini Algeria jana walisikika katikati ya mji mkuu wa nchi hiyo wakipiga nara " hakuna uchaguzi kesho" huku wakiwa wamebeba mabango yanayosomeka" mmeharibu nchi." Polisi walikuwa wamesimama ili kuzuia barabara huku helikopta zikipita katika anga ya mji mkuu huo.
Wananchi wa Algeria wanasema kuwa hakuna uchaguzi utakaokuwa huru au wa kiadilifu nchini mwao wakati viongozi wa utawala wa zamani wa nchi hiyo wangali madarakani huku jeshi likiendelea kujihusisha na masuala ya kisiasa. Wanasema kuwa wanataka kutekelezwa mageuzi makubwa nchini humo. Habari zinasema kuwa hadi sasa hakuna wasimamizi wa uchaguzi wa nje waliofika kwa ajili ya kusimamia uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇