Timu
ya Taifa ya mchezo wa kuogelea (The Tanzanite) wakiwa katika pozi baada
ya kushinda nafasi ya tatu katika mashindano ya Afrika ya Kanda ya Tatu
yaliyomalizika Jumapili mjini, Nairobi, Kenya.
Na Mwandishi wetu
Dar
es Salaam. Timu ya Taifa ya mchezo wa kuogelea ya Tanzania (The
Tanzanite) imeshinda kombe la Shaba katika mashindano ya Kanda ya Tatu
Afrika yaliyomalizika jijini Nairobi, Jumapili jioni.
Tanzania
iliyowakilishwa na waogeleaji 25 imemaliza katika nafasi ya tatu
katika mashindano hayo yaliyoshirikisha nchi tisa za Afrika kwa
kukusanya jumla ya pointi 2, 044.50.
Wenyeji, Kenya ilimaliza katika nafasi ya kwanza kwa kupata pointi 2, 447.50 na kufuatiwa na Uganda iliyopata pointi 2, 392.
Mbali
ya kushinda nafasi hiyo, waogeleaji watatu wa Tanzania, Sydney
Hardeman, Romeo Mihaly na Sylvia Caloiaro walishinda vikombe kwa kushika
nafasi ya kwanza kwa waogeleaji wa wenye miaka yao.
Sydney
alipata pointi 130 kwa waogeleaji wenye miaka kati ya 11-12 wakati
Romeo alikusanya pointi 118 katika umri huo huo na Sylvia alipata pointi
126.
Kwa
mujibu wa matokeo hayo, waogeleaji wa kike wa Tanzania waling’ara zaidi
kwa kumaliza katika nafasi ya pili kwa kukusanya pointi 1,083 huku
wenyeji, Kenya wakishika nafasi ya kwanza kwa kupata pointi 1,180 na
Uganda katika nafasi ya tatu kwa kupata pointi 851.
Kwa
upande wa wanaume, Tanzania ilikusanya pointi 865.5 na kushika nafasi
ya tatu nyuma ya Kenya iliyomaliza ya pili kwa kupata pointi 1, 143.50
na Uganda iliyokuwa ya kwanza kwa kupata pointi 1, 421.
Matokeo
yanaonyesha kuwa Afrika Kusini imeshika nafasi ya nne kwa kupata pointi
1, 540 wakati nafasi ya tano imekwenda kwa Zambia kwa kupata pointi
1,386 na Burundi ya sita kwa kupata pointi 866.
Waliokuwa
mabingwa watetezi, Sudan imeshindwa kufukuta baada ya kushika nafasi ya
saba kwa kupata pointi 812 huku Djibouti ikipata pointi 105 na Malawi
ikipata pointi 88.
Timu
ya Tanzania iliundwa na waoegeleaji Maria Bachmann, Sylvia Caloiaro,
Kayla Temba, Sydney Hardeman, Linnet Laiser, Sophia Latiff, Sarah
Shariff, Avalon Fischer, Nawal Shebe, Roos Nevelsteen, Eunike Mathayo na
Lissa Stanley.
Wengine
ni Mischa Ngoashani, Augustino Lucas, Romeo Mihaly, Delhem Rashid,
Terry Tarimo, Aaron Akwenda, Singko Steiner, Ethan Alimanya, Sil
Kleinveld, Ezra Miller, Augustino Lucas, Ashraf Moez, Nathan Kagoro,
na Peter Itatiro.
Meneja
wa timu hiyo Hadija Shebe aliwapongeza waogeleaji hao kwa matokeo hayo
mazuri pamoja na changamoto mbalimbali abazo zilisababisha baadhi ya
waogeleaji kushindwa kushiriki.
Hadija
alisema kuwa walipanga kuwa na waogeleaji 27, lakini waogeleaji wawili,
Collins Saliboko anayesoma nchini Uingereza na Hilal Hilal anayesoma
Dubai wameshindwa kushiriki kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo
wao.
“Matokeo
yanaonyesha jinsi gani Tanzania inafanya vyema katika mchezo huo na
tunawaomba wadau watusaidie kwani bila wafadhiri, mchezo hauwezi kufikia
hatua ya juu kabisa ya maendeleo,” alisema Hadija.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇