Jaji
Mkuu wa Mahakama Kuu, Zanzibar, Omary Othman Makungu (kulia)
akimsikiliza Mwenyekiti wa THBUB, Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu
aliyemtembelea ofisini kwake
Desemba 2, 2019. Wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa THBUB,
Mohamed
Khamis Hamad.
Na Mbaraka Kambona.
Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu, Visiwani Zanzibar, Omary Othman Makungu amemueleza
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji Mstaafu Mathew
Mwaimu kuwa wako tayari kushirikiana tume kutatua kero za wananchi zinazohusu
upatikanaji wa haki nchini.
Jaji Makungu alisema hayo alipokutana na Mwenyekiti wa tume ofisini kwake Visiwani
Zanzibar Desemba 2, 2019.
Makungu alitoa ahadi hiyo ya ushirikiano kufuatia Mwenyekiti wa tume kumuomba
kusaidia katika kutatua malalamiko mbalimbali ya kudai haki yanayopelekwa tume kuhusu
Mahakama.
Awali akitoa maelezo, Mwenyekiti wa tume alimwambia Jaji Makungu kuwa katika kazi zao
wamekuwa wakipata changamoto nyingi zinazohusiana na Mahakama, hususani mahakama
za mwanzo kuchelewa kushughulikia utoaji wa nakala za hukumu ya kesi, ucheleweshwaji
wa kesi na mahabusu kukaa muda mrefu bila kesi zao kusikilizwa.
Jaji Mwaimu alimueleza Makungu kuwa wamekuwa wakipata sana malalamiko hayo na
mara kadhaa wakiwasiliana na mamlaka husika ili kupata majibu kumekuwa na tabia ya
kutojibu barua wanazowaandikia.
“Tunakuomba Mheshimiwa Jaji kwa huku Zanzibar utusaidie kwa hili, tunaomba ushirikiano
wako ili wananchi wapate haki zao kwa wakati, maana tusiposhirikiana kutoa majibu kwa
wakati inapelekea haki iliyostahili kuchelewa na inapoteza maana”alieleza Jaji Mwaimu
Wakati akitolea ufafanuzi wa maelezo ya Mwenyekiti wa tume, Makungu alisema ni wazi
kuwa Mahakama ni mdau mkubwa wa tume na hawana budi kufanya kazi kwa kushirikiana.
“Niwahakikishie tu, kuwa tutatoa ushirikiano kwa tume, imekuwa ni utaratibu wangu kila
mwaka kutembelea Magereza, huwa nawachukua na mahakimu kwenda kusikiliza
malalamiko ili wajue wanawajibu kiasi gani kwa wananchi”alisema Makungu
“Ni lazima tufanye kazi vizuri, tushirikiane ili tuweze kuisaidia serikali, ni muhimu kuwa na
makubaliano, inabidi tupange kikao kazi tukae kwa pamoja ili tuwekane sawa”alimaliza Jaji
Makungu
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇