LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 3, 2019

MAKUMI WAPOTEZA MAISHA NA WENGINE KUJERUHIWA

Watu wasiopungua 42 wamepoteza maisha na kujeruhiwa katika ajali mbaya ya basi kaskazini mwa Tunisia.
Vyombo vya habari vimeripoti habari hiyo na kufafanua kwa kusema, ajali hiyo mbaya imetokea baada ya basi hilo kutumbukia kwenye bonde lenye kina kirefu huko Ain Snoussi.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Tunisia imethibitisha habari hiyo na kusema kuwa, basi hilo lilikuwa na watu 43, liliacha njia na kugonga kingo za chuma pembeni mwa barabara na kutumbukia bondeni katika eneo hilo lililoko karibu na mpaka wa Algeria. Basi hilo lilikuwa linaelekea kwenye eneo la utalii la milimani la Ain Draham.
Magari ya Wagonjwa Tunisia yaliyotumika kuchukua wahanga wa ajali hiyo mbaya

Wizara ya Afya ya Tunisia imesema kuwa, wahanga wa ajali hiyo mbaya walikuwa na umri wa baina ya miaka 20 hadi 30. Majeruhi wamewahishwa kwenye hospitali za karibu na eneo hilo.
Hata hivyo hadi wakati inaripotiwa habari hii kulikuwa hakujatangazwa sababu za ajali hiyo, ingawa ukweli ni kwamba barabara hasa za mikoani nchini Tunisia ni nyembamba na za hatari mno hususan zile zinazopita kwenye kingo za mabonde milimani.
Rais Kais Saied wa Tunisia pamoja na Waziri Mkuu, Youssef Chahed wametembelea eneo la tukio hilo ambalo ni maarufu kwa jina la eneo kifo. Ajali hiyo inahesabiwa kuwa miongoni mwa ajali mbaya zaidi ya barabarani kuwahi kutokea katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.
Tunisia ni ya pili kwa kuwa na rekodi mbaya ya ajali za barabarani kaskazini mwa Afrika ukitoa Libya. Hayo ni kwa mujibu wa uchunguzi wa Shirika la Afya Duniani , WHO uliofanywa mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages