Serikali
ya Awamu ya Tano imeuwezesha mkoa wa Mara kujenga Hospitali 4 za
Wilaya, Vituo vya Afya 13 kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za
afya kwa wananchi.
Akizungumza katika kipindi cha ‘TUNATEKELEZA’ Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Adam Malima amesema mkoa huo umepiga hatua kubwa katika kuimarisha huduma mbalimbali za jamii ikiwemo sekta ya afya kutokana na kutekelezwa kwa ujenzi wa miundombinu ya sekta hiyo kwa ufanisi.
“Mradi
wa Hospitali ya Kanda ya Mwalimu Nyerere unaendelea vizuri na
utawezesha wananchi kupata huduma za kibingwa ikiwemo za mifupa na
nyingine hali itakayoondoa adha ya wananchi kusafiri hadi Hospitali ya
Bugando kufuata huduma hizo” Alisisitiza Malima.
Akifafanua amesema kuwa mkoa huo umepata mafanikio makubwa katika sekta nyingine
kama vile elimu kwa kujenga miundombinu ya kisasa yakiwemo madarasa na
maabara hali iliyochangia kukua kwa kiwango cha elimu katika mkoa huo
ikilinganishwa na miaka iliyotangulia kabla ya uwekezaji huo.
Kwa
upande wa sekta ya madini amesema kuwa kuwepo kwa sheria nzuri na
taratibu zilizowekwa na Serikali ya Awamu ya Tano, mkoa huo umezalisha
kilo 130 za dhahabu kufikia Septemba mwaka huu hali inayochangia kukuza
sekta ya madini na uchumi kwa ujumla.
Akizungumzia
mikakati yake ya kukuza kilimo na uvuvi, Mhe. Malima amesema kuwa
dhamira ya mkoa huo ni kuona sekta hizo zinatoa mchango stahiki katika
uchumi kutokana na hatua zilizochukuliwa katika kokomesha uvuvi haramu
katika mkoa huo.
Aidha,
Mhe. Malima amebainisha kuwa wamejipanga kukuza sekta ya utalii katika
mkoa huo ili kuongeza pato la mkoa huo hatua itakayowasaidia kuwainua
wananchi kiuchumi na Taifa kwa ujumla.
Kipindi
cha ‘TUNATEKELEZA’ kinarushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)
na kuratibiwa na Idara ya Habari MAELEZO ambapo awamu hii
inawashirikisha wakuu wa mikoa yote Tanzania Bara.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇