LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 1, 2019

CCM YASHIRIKI SAFARI YA MAJARIBIO YA TRENI YA ABIRIA KUTOKA DAR ES SALAAM KWENDA MOSHI KILIMANJARO

CCM Blog, MOSHI
Baada ya safari za treni ya abiria za Dar es Salaam na Moshi mkoani Kilimanjaro kusimama kwa miaka 25, safari ya kwanza ya majaribio ya treni hiyo imeanza leo, Disemba Mosi, 2019, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akishiriki katika safari hiyo. 

"Kuanza kwa safari hii ya majaribio kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi, Kilimanjaro ni sehemu ya Maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2015-2020 katika eneo la usafiri na usafirishaji wa watu na mizigo ambapo miradi mikubwa mitatu inatekelezwa kwa pamoja ikiwamo ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa (standard gauge railway -SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Makutopola, Dodoma, awamu ya kwanza.

Maboresho makubwa ya reli ya kati kutoka Dar es Salaam hadi Isaka ili kuiongezea ufanisi na ubebaji mzigo mkubwa zaidi pamoja na ufufuaji na ukarabati mkubwa wa reli njia ya kaskazini inayojumuisha Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga na Kilimanjaro awamu ya kwanza", amesema Polepole. 

Polepole amepongeza uongozi wa Shirika la Reli kwa kuipanga kwa mafanikio safari hiyo ya kwanza ya treni ya abiria na ametoa rai kwa vyombo vya ulinzi na usalama na Shirika kuimarisha ulinzi na kutoa elimu ya ujirani wema kati ya reli na jamii ziishizo pembezoni mwa reli ili kuitunza na kuilinda reli hii muhimu kwa maendeleo.

Katika safari hiyo ya kwanza ya majaribio imetumia cha kisasa cha treni “9013 Classic” na ikiwa imefunga mabehewa tisa yakiwamo ya daraja la kwanza, la pili, la tatu, behewa lenye mgahawa  wa vyakula na vinywaji baridi na vikali pamoja na behewa la uendeshaji, usalama na usimamishaji wa treni.

Pamoja na Polepole, watendaji wa Shirika la Reli wameongozwa na Masanja Kadogosa, Mkurugenzi Mkuu wa TRC na Maafisa waandamizi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa usafiri wa ardhini (LATRA).

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages