KWA
zaidi ya Muongo mmoja sasa, Mitandao ya kijamii imetumika kama njia ya
mawasiliano kwa marafiki zetu tuliopotezana siku nyingi mitandao imekuwa
zana ya kupata taarifa iwe kuhusu biashara, jabari, masoko hata utani;
watu ulimwenguni pote wanatumia mitandao ya kijamii kwa madhumuni
mbalimbali na kupatikana kwake ni rahisi kuliko hapo nyuma, na kuna
nchi na baadhi ya maeneo imefikiwa zaidi na mitandao kuliko kwingine.
Takwimu
zinaonyesha kwamba, matumizi ya mitandao ya kijamii yamekuwa ni njia
bora ya Kidigitali ya masoko ya Kimataifa na hiyo ni kutokana na namna
inavyoweza kutangaza na kukuza masoko ndani na nje ya nchi pamoja na
uteuzi wa mtandao upi ambao utafikisha taarifa kwa haraka na kuleta
matokeo chanya.
Ni nchi gani zinatumia zaidi mitandao ya Kijamii?
Umewahi
kujiuliza au kudadisi kuwa ni nchi ipi ni kinara wa mitandao ya
kijamii? Ufilipino ndio nchi yenye watu wanaotumia zaidi mitandao ya
kijamii. Mpaka kufikia mwaka 2018, Ripoti ya Masuala ya Digitali ya
Ulimwengu(Global Digital Report) iliitaja Ufilipino kama mtumizi mkuu wa
mitandao ya kijamii. Ni kwa miaka miwili, Ufilipino imebaki kuwa
kinara.
Watumiaji
wa Mitandao huko Ufilipino wanatumia wastani wa saa 3 na dakika 57 kila
siku kwenye mitandao ya kijamii. Hii ni theluthi moja tu ya muda ambao
wanatumia inteneti kila siku (Saa9 na dakika 29) na kuifanya Ufilipino
kuwa nchi ya pili kwa matumizi ya inteneti baada ya Thailand.
Wakazi
milioni 67 nchini humo wanatumia mtandao wa Facebook sambamba na
wengine milioni 10 wanaotumia Instagram. Asilimia 10% ya watumiaji wa
Mitandao ya kijamii pia ni watumiaji wa YouTube ndani ya Taifa hilo.
Kwa ujumla, Bara la Asia lina watumizi wengi wa mitandao ya kijamii kwa kiasi kikubwa.
Kwa
ufupi huu ndio muda watu hutumia mitandao ya kijamii kulingana na
Ripoti ya Masuala ya Digitali ya Ulimwengu(Global Digital Report) 2018
Indonesia – Saa 3 na dakika 23, hii ni nchi ya tatu ulimwenguni kwa wastani wa matumizi ya mitandao ya kijamii.
Thailand – Saa 3 na dakika 10, inashika namba 4 ulimwenguni kwa wastani wa matumizi ya mitandao ya kijamii.
Malaysia – Saa 3 kila siku, inatajwa kuwa nambari 8 Ulimwenguni
Umoja wa Falme za Kiarabu, Emerati- saa 2 na dakika 56 ikishika namba 9 ulimwenguni.
Mitandao
ya Kijamii imeendelea kutumika zaidi barani Asia hasa Saudi Arabia,
ambayo imeonesha maendeleo makubwa, kati ya Januari 2017 na 2018,
Matumizi ya mitandao yaliongezeka kwa asilimia 32, asilimia moja zaidi
mbele ya India. Indonesia ikiwa na asilimia 23 na Vietnam 20.
Vipi kuhusu Marekani na Canada?
Ungetarajia
kuwa Marekani ingekuwa juu zaidi katika matumizi ya mitandao kwa kuwa
ndipo mitandao hii inapozaliwa, Sivyo? Ushahidi unaonyesha kwamba,
Marekani haikaribii hata kidogo takwimu za matumizi ya inteneti na
mitandao kama ilivyo kwa Asia.
Marekani
ni nchi ya 24 kwa wastani wa matumizi ya saa 2 na dakika 1 tu kwa siku,
wakati huo huo, Canada ipo nafasi ya 30 Ulimwenguni kwa wastani wa saa 1
na dakika 48 na hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Global Digital Report ya
2018 iliyoeleza kwamba nchi zote mbili hazina idadi kubwa ya watumiaji
wapya. Januari 2017 na Januari 2018, kulikuwa na watumiaji wapya kwa
asilimia 9 nchini Canada na asilimia 7 nchini Marekani.
Kwa
kuwa mitandao ya kijamii ilianza kuwa maarufu Marekani na intaneti
yenye kasi zaidi, inafanya uwekaji wa vitu mitandaoni kuwa wa haraka na
na hivyo muda mchache kutumika kulinganisha na maeneo mengine.
Kulingana
na kituo cha Utafiti cha Pew, Mitandao ya Kijamii imekuwa ni muunganiko
wa tabia zinazoibuka na zile za umaarufu ambazo zimekuwepo kwa kipindi
kirefu ndani ya Marekani. Facebook na YouTube zinatumika zaidi, angalau
73% ya watu wazima wote hupachika maandiko kwenye Facebook, na 68%
kutazama video kwenye YouTube. Vijana wengi kati ya umri wa miaka 18 had
24, wanatumia Snapchat kwa 78%, na 71% huingia mara tatu kwenye mtandao
huo kila siku. Pia kuna 71% ya vijana ambao hutafuta au kupakia picha
kwenye mtandao wa Instagram, 29% hutumia Pinterest na karibu 25% hutumia
mtandao wa kibiashara na kazi wa LinkedIn.
Huko
Canada, Facebook imekuwa mtawala zaidi kuliko hata ilivyo Marekani.
Mamlaka ya Uthibiti ya Canada (Canadian Internet Registration
Authority-CIRA) inaeleza kwamba 77% ya wakanada wote wapo Facebook.
Lakini baada ya Facebook raia wa Canada wanapendelea mitandao ya
Instagram na LinkedIn (35%), kisha mtandao wa Twitter (26%), na Snapchat
(19%). Canada ni namba tatu kwa umaarufu wa shughuli za mitandaoni, na
kuifanya mtumizi mkubwa wa Inteneti karibu 67%.
Kupokelewa kwa Mitandao ya Kijamii
Ukitazama
ulinganifu wa matumizi ya mitandao ya kijamii, utajiri wa Taifa Fulani
sio kigezo kabisa, Unaweza kufikiri nchi tajiri ndio itakuwa na
watumiaji wakubwa wa mitandao. Sivyo, na sio lazima iwe hivyo.
Nchi
za Mashariki ya Kati zina sifa ya uchumi ambao unaendelea, Lakini
Ukanda huo una matumizi makubwa ya Mitandao ya Kijamii kuliko pengine
popote. Pew Research Center inaeleza kwamba 75% ya watu wa Jordan
wanatumia mitandao ya kijamii, Lebanon ni 72%.
Nchi
zenye uchumi imara zina matumizi madogo ya mitandao ya kijamii, mfano
Ujerumani ni 40% na Japani ni 39%. Hii ni chini wa Wastani wa matumizi
ya mitandao ya kijamii ulimwenguni ambayo ni 53%.
Uingereza
pia watu wanatumia muda mchache kati katika mitandao ya kijamii
kulinganisha na Marekani ingawa 85% ya watu wote wanatumia mitandao.
Ripoti
za hivi karibuni zinaonesha kwamba Facebook, Facebook Messenger,
WhatsApp, na Instagram inatumiwa sana Uingereza ingawa Facebook
inatumika zaidi lakini Instagram na WhatsApp zimejikusanyia watumiaji
wengi miaka ya karibuni.
Jambo
lingine muhimu ni kwamba, katika nchi zilizoendelea, Wanawake wanatumia
zaidi Mitandao kuliko wanaume. Mfano Sweden, Wanawake wanaotumia
mitandao ni 72% ukilinganisha na Wanaume ambao ni 63%. Ingawa Wanaume
wanatumia zaidi intaneti kwa 94% huku wanawake ni 90%
Kwa nini Mataifa yanatumia Mitandao ya Kijamii?
Sababu
kubwa ya Ufilipino kuwa na matumizi makubwa ya Mitandao ni idadi kubwa
ya watumiaji wanaopakia maandiko kila kukicha lakini pia idadi kubwa ya
watu wanaoitembelea nchi hiyo.
Huko
Ulaya, Wengi hupata habari kupitia mitandao mfano tu, Nchini Italia,
Nusu ya Raia wote wanatumia mitandao kupata Habari. Angalau 40% ya watu
wanapata habari kupitia mitandao katika nchi hizi Uhispania, Denmark,
na Sweden. Facebook ndio inatumika zaidi kupata Habari mbalimbali.
Ikiwa
na mionekano mipya na ya kuvutia, Wafanyabiashara wengi sasa wanaitumia
Mitandao kuwasiliana na wateja wao. Nchi kadhaa zinatumia Mitandao kwa
biashara. Ingawa sababu za matumizi ya mitandao zinatofautiana kulingana
na watumiaji, ukubwa wa matumizi na mengineyo lakini ukweli ni Kwamba
mitandao imekuwa na thamani kubwa sana wakati huu kuliko kipindi
chochote kihistoria.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇