UTAFITI
uliyofanywa na Shirika linalohusika na usalama na Ustawi wa wanyama
Duniani (World Animal Protection) umebaini kuwa kuku wengi wanaouzwa
katika maeneo mbalimbali nchini wakidaiwa kuwa ni wa kienyeji si wa
kienyeji kama inavyosemwa.
Utafiti
huo umebaini kuku hao si wa kienyeji bali ni kuku wa kisasa maarufu
kama kuku wa kizungu wanaofungwa majumbani kwa kupewa majani pamoja na
dawa mbalimbali za kuwakuza na kuwafanya kuwa wagumu.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam leo wakati akiwasilisha ripoti ya utafiti huo
uliyofanywa katika nchi nne Tanzania ikiwamo, Msemaji Mkuu wa Shirika
hilo, Victor Yamo alisema utafiti huo ambao ulifanywa Juni hadi Julai
mwaka huu katika mikoa ya Arusha na Dar es Salaam umebaini jambo hilo
hivyo watumiaji wanapaswa kuwa makini.
Yamo
amesema kuku wengi wanauzwa katika mikoa hiyo wamekuwa wakupewa dawa za
kuwakuza ambazo zina madhara kwa binadamu pindi wanapotafuna mifupo yao
"Wakati
watu wetu wakitembelea kwenye masoko mbalimbali kuulizia bei ya kuku na
wakabaini uwepo wa kuku wa kisasa wengi na mwananchi uuziwa kwa kuambia
kuwa ni wa kienyeji jambo ambalo ni uongo," alisema.
Amesema
utafiti huo ulifanyika kwa lengo la kujua walaji wananunua nyama za
aina gani, kutoka wapi pamoja na kuangalia kama wanafahamu ubora wa
chakula na matumizi ya dawa za wanyama.
"Tunaamini
kuwa mteja ataelewa nyama anayotaka kununua au kula inaubora au tatizo
kiasi gani itakuwa rahisi kujiepusha nayo na kutafuta kitu kingine
mbadala cha kula," alisema
Aidha
Yamo amesema kwa sasa Shirika lao linafanya jitihada kubwa kuhakikisha
linaimarisha ustawi na haki za wanyama na sheria za kuwalinda wanyama
hao zinapitishwa na serikali husika katika kila nchi.
Amesema
pamoja na kuyafanya hao wanatoa wito kwa watanzania waanze kuelewa kuwa
kama watashindwa kuangalia ustawi wa wanyama hasa wanaoliwa kuna hatari
kubwa ya kupotea.
"Ni
ukweli uliyowazi kuwa ustawi wa wanyama ni muhimu sana na kwa kutambua
hilo tumekuwa tukienda mashuleni kufundisha jambo hilo na masuala ya
usalama wa chakula na ubora wa dawa," alisema.
Mtaalamu
wa masuala ya kutetea Haki na Ustawi wa Wanyama kutoka shirika la World
Anima Protection ,Dkt Victor Yamo akizungumza na Waandishi wa habari leo
jijini Dar,alipokuwa akiwasilisha ripoti ya utafiti uliyofanywa katika
nchi nne Tanzania ikiwamo, kuhusu kubainika kwa kuku wengi wanaouzwa
katika maeneo mbalimbali nchini wakidaiwa kuwa ni wa kienyeji kumbe si
wa kienyeji kama inavyosemwa.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza mtaalamu huyo wa Haki
na Ustawi wa Wanyama kutoka shirika la World Anima Protection ,Dkt
Victor Yamo alipokuwa akiendelea kufafanua mambo mbalimbali yahusuy haki
na ustawi wa Wanyama nchini Tanzania
Mtaalamu
wa masuala ya kutetea Haki na Ustawi wa Wanyama kutoka shirika la World
Anima Protection ,Dkt Victor Yamo akifafanua jambo kwa msisitizo mbele
ya Waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar,alipokuwa
akiwasilisha ripoti ya utafiti uliyofanywa katika nchi nne Tanzania
ikiwamo, kuhusu kubainika kwa kuku wengi wanaouzwa katika maeneo
mbalimbali nchini wakidaiwa kuwa ni wa kienyeji kumbe si wa kienyeji
kama inavyosemwa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇