LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 2, 2019

MAPIGANO MAKALI YAMEZUKA LEO DR

  • Mapigano makali yamezuka leo Kongo DR, maandamano dhidi ya Monusco yanaendelea
Watu wasiopungua wawili wameripotiwa kuuawa baada ya mapigano makali kutokea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrsia ya Kongo leo Jumatatu huku maandamano ya wananchi wa Beni ya kutaka askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa waondoke nchini humo kutokana na kushindwa kuwalinda raia yakiwa yanaendelea.
Askari wa kulinda usalama wamewazuia mamia ya waandamanaji waliokuwa wanajaribu kuingia kwenye eneo la askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa (Monusco) ndani ya uwanja wa ndege karibu na mji wa Beni ambalo ni moja ya kambi mbili za askari wa Umoja wa Mataifa katika eneo hilo.
Maafisa wa hospitali moja iliyopokea wahanga wa mashambulizi ya leo wamenukuliwa wakisema kuwa bado mapigano makali yanaendelea. Watu wawili wameuawa ambao ni mtoto mmoja mdogo wa kiume na mwanamke mmoja. 

Askari wa Monusco


Wananchi wa Beni wanasema kuwa hawahisi kuwa na usalama wowote, hivyo lazima askari wa Umoja wa Mataifa waondoke eneo hilo. Wananchi hao wamesisitiza kuwa wataendelea na maandamano hayo hadi pale askari wa mwisho wa Umoja wa Mataifa atakapoondoka kwenye eneo hilo.
Wananchi wenye hasira walimiminika barabarani wiki iliyopita kulalamikia udhaifu wa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa baada ya waasi kufanya mauaji makubwa ya halaiki katika eneo lililoko karibu na Oicha, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Siku ya Ijumaa, wanavijiji wasiopungua 19 waliuliwa kwa umati na waasi wanaoaminika kuwa na wa ADF wenye ngome zao ndani ya misitu iliyoko kwenye mpaka wa Uganda. Wengi wa wahanga hao waliuawa kwa kukatwa katwa kwa mabanga au kukata vichwa na waasi hao. Tarehe 24 Novemba pia, wakazi wengine wanane wa Beni waliuliwa kama hivyo na waasi hao.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages