LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 11, 2019

KAHATANO: UFUATILIAJI MWENDO KASI WA MABASI UPO PALE PALE, ATAKAYEKIUKA KUKIONA CHA MTEMA KUNI


Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa Barabara Johansen Kahatano kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA)akizungumza na Mabalozi wa Usalama barabarani RSA pamoja wageni kutoka  Jumuiya ya Asasi za Kiraia kutoka Pemba (PSCSO)wakiwa katika  stendi kuu ya mabasi Ubungo Jijini Dar es salaam zowezi la Abiria Paza sauti katika.
Mwenyekiti wa Mabalozi wa Usalama barabarani John Seka akiteta jambo na Mkurugenzi wa udhibiti wa Usafiri wa Barabara wa Mamlaka ya Usafiri Ardhini (LATRA) Jahansen Kahatano katika Stendi kuu ya Mabasi yaendayo mkoani na nchi jirani Ubungo.
Mkurugenzi wa udhibiti wa  Usafiri wa Barabara  wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) Jahansen Kahatano katika Stendi kuu ya Mabasi yaendayo mkoani na nchi jirani Ubungo.Mabalozi wa usalama barabarani Tanzania RSA,pamoja  wageni kutoka  Jumuiya ya Asasi za Kiraia kutoka Pemba (PACSO)mara baada ya kuendesha zowezi la Abiria Paza sauti katika stendi kuu ya mabasi Ubungo Jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Tafiti za kisheria  RSA Augustus Fungo akieleza wageni kutoka  Jumuiya ya Asasi za Kiraia kutoka Pemba (Pacso) kuja Tanzania bara kujifunza namna RSA inavyoendesha shughuli zao za usalama barabarani na namna ilivyofanikiwa kiutendaji

Nuru Hatibu Hussein mkaguzi wa wamagari stendi kuu ya Mabus Ubungo akiwa anatoa ufafanuzi kuhusiana na majukumu yao ya kila siku katika stendi hiyo kabla na magari kuanza safari kuelekea mikoani.

Mkurugenzi Mtendaji wa Pemba Association for Civil Society Organization (PACSO )akizungumza mara baada ya zoezi la abiria paza sauti lililoendeshwa na Mabalozi wa usalama barabarani stendi kuu ya mabasi Ubungo na kuwashirikisha wageni kutoka Pemba.

Majira Kafumu Mweyekiti wa umoja wa madereva wa mabasi makubwa nchini Tanzania UWAMATA akizungumza na mabalozi wa usalama barabarani pamoja na wageni kutoka PACSO
Wa tatu kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa RSA Taifa John Seka ,aliyepo kulia kwake ni Elias Xavier ambaye ni Mshauri Muelekezi kutoka Asasi ya Foundation for Civil Society( FCS)Kushoto kwake ni Katibu Umoja wa madereva wa mabasi makubwa Tanzania,wa pili kutoka kushoto ni mmoja kati ya wageni kutoka Pemba waliokuja kupata uzoefu namna RSA inavyoendesha sughuli zake.
Picha baadhi ya wageni kutoka  Jumuiya ya Asasi za Kiraia kutoka Pemba (Pacso)wakiwa katika  stendi kuu ya mabasi Ubungo Jijini Dar es salaam zowezi la Abiria Paza sauti katika
Mabalozi wa usalama barabarani Tanzania RSA wakiwa katika picha ya pamoja  wageni kutoka  Jumuiya ya Asasi za Kiraia kutoka Pemba (Pacso)mara baada ya kuendesha zowezi la Abiria Paza sauti katika stendi kuu ya mabasi Ubungo Jijini Dar es salaam
Mabalozi wa usalama barabarani Tanzania RSA wakiwa katika picha ya pamoja  wageni kutoka  Jumuiya ya Asasi za Kiraia kutoka Pemba (Pacso)mara baada ya kuendesha zowezi la Abiria Paza sauti katika stendi kuu ya mabasi Ubungo Jijini Dar es salaam
Mabalozi wa usalama barabarani Tanzania RSA wakiwa katika picha ya pamoja  wageni kutoka  Jumuiya ya Asasi za Kiraia kutoka Pemba (Pacso)mara baada ya kuendesha zowezi la Abiria Paza sauti katika stendi kuu ya mabasi Ubungo Jijini Dar es salaam
Mabalozi wa usalama barabarani Tanzania RSA wakiwa katika picha ya pamoja  wageni kutoka  Jumuiya ya Asasi za Kiraia kutoka Pemba (Pacso)mara baada ya kuendesha zowezi la Abiria Paza sauti katika stendi kuu ya mabasi Ubungo Jijini Dar es salaam.

Na.Vero Ignatus 

Mabalozi wa usalama barabarani Tanzania RSA kwa kushirikiana na Jumuiya ya Asasi za Kiraia kutoka Pemba (Pacso)wameendesha zowezi la Abiria Paza sauti katika stendi kuu ya mabasi Ubungo Jijini Dar es salaam lengo likiwa ni kutoa elimu kwa abiria kutoa taarifa pale wanapoona ukiukwaji na uvunjifu wa sheria za usalama barabarani 

Elimu hiyo inamsaidia abiria kutambua kuwa anatakiwa kuripoti vitendo vyovyote vinavyohatarisha usalama wake ,wa chombo pamoja na usalama wa anachosafiria,mwendokasi,ulevi wa dereva,upitaji wa hatari wa magari mengine bila kufuata sheria na alama za barabarani ,dereva kuzungumza na simu akiwa anaendesha,pamoja na kuripoti lugha chafu na uhasama kwa abiria 

Akizungumza Mkurugenzi wa Udhibiti wa usafiri wa Barabara wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini(LATRA) Johansen Kahatano amesema utaratibu wa kufuatilia mwendokasi wa mabasi ya abiria haujasitishwa upo na unaendelea kutumika na wanaendelea kuwafuatilia wahusika na watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria.

Amesema kuwa kwa kushirikiana na Asasi za kiraia ambazo zinashughulika na masuala ya usalama barabarani ikiwemo RSA, zimekuwa msaada wa mkubwa kwani zimekuwa zikitoa elimu kwa abiria kufahamu wajibu wao wa msingi wawapo ndani ya chombo cha usafiri,katika kuripoti vitendo vyovyote vinavyohatarisha usalama wa gari na abiria kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tafiti za kisheria  RSA Augustus Fungo amesema kuwa wa wageni hao walikuja Tanzania bara kujifunza namna RSA inavyoendesha shughuli zao za usalama barabarani na namna ilivyofanikiwa kiutendaji.

Fungo amesema RSA ilipokea jumla ya wageni 21 kutoka Pemba kutoka kwenye muunganiko wa Asasi 93 ambapo zinaunda  PACSO ambapo zimekuja Asasi 14 kwaajili ya kubadilishana ujuzi hususani katika maswala ya mitandao.

Akizumzia juu ya safari yao Mkururugenzi Mtendaji wa PACSO Mohamed Najim amesema wamejifunza mambo mengi haswa namna Taasisi ya RSA inavyofanya kazi kwa kwakujitolea na mooyo wa kufanya kazi kwa pamoja na utendaji kazi.

Amesema wameshangazwa na utendaji kazi wa Askari namna wanavyokagua magari kabla hayajaanza safari jambo ambalo Zanzibar ni  nadra sambamba na abiria wanavyopewa uhuru wa kujieleza tofauti na Zanzibar wanaangalia zaidi wamiliki.

''Tukifika Zanzibar tunaenda kukaa na  kufanya mkutano na Chama cha Usafirishaji cha Pemba (PESTA)ili tuweze kuwashirikisha yale tuliyojifunza Tz bara kwajili ya mabadiliko''

Kwa upande wake mkaguzi wa magari stendi kuu ya ubungo Nuru Hatibu Hussein amesema kuwa kazi yao kubwa ni kukagua magari kabla ya kuanza safari kuangalia mifumo yake injini,mwendo,gari litakalikutwa na linahitilafu wanaliweka pembeni kwaajili ya matengenezo,gari ambalo linahitilafu kubwa halitaruhusiwa kuendelea na safari badala yake wanawapa muda kisheria kwa masaa manne kurekebisha dosari zilizopo ikishindikana wanabadilisha gari au kurudisha nauli za abiria.

Aidha amesema zipo changamoto kubwa wanazokabiliana nazo haswa wakati wa kukagua magari hayo kwani hakuna sehemu muhimu iliyotengwa kwaajili ya kukagulia magari hao ,bali inawaazimu kulala chini ya gari ili waweze kulikagua huku dereva akiwa ndani jambo ambalo wakati mwingine ni hatarishi kwa maisha yao.  

Zoezi hilo la abiria paza sauti lilifanyika mwishoni mwa juma na kushirikisha Taasisi ya RSA,Asasi za Kiraia kutoka Pemba (PACSO)Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani pamoja na LATRA

Sheria ya usalama barabarani ya mwaka sura ya 168 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002 inamtaka kila mtumiaji wa barabara kufahamu sheria na kuelewa namna matumizi bora ya barabara kwa nia ya kuepuka kuvunja sheria pamoja na kuepuka ajali kutokana na matumizi mabaya ya barabara 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages