Na Bashir Nkoromo, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeamuru Makatibu Wakuu wake wa zamani, Abdulrahman Kinana na Mzee Yusuf Makamba pamoja na Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe waitwe na Kamati ya Usalama na Maadili ya Taifa ya CCM ili wajibu tuhuma za kimaadili zinazowakabili kwa mujibu wa Katiba ya Chama na Kanuni ya Maadili na Uongozi
Amri hiyo imetolewa na kupitishwa na Wajumbe, katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, kilichofanyika kwa mara ya kwanza jijini Mwanza chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Idara ya Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole imesema Halmashauri Kuu hiyo ya Taifa (NEC) ya CCM pia imepokea, kujadili na kuridhia kwa kauli moja Taarifa ya Kamati ya Usalama na Maadili juu ya uamuzi wa Mwenyekiti wa CCM wa kuwasamehe wanachama walioomba radhi kwake baada ya kukiri mbele yake kufanya makosa ya kimaadili yaliyokidhalilisha chama na viongozi wake mbele ya umma.
Taarifa hiyo imewataja wanachama hao kuwa ni Mbunge wa Bumbuli Januari Makamba, Mbunge wa Mtama Nape Nnauye na Mbunge wa Sengerema William Ngeleja.
"Kikao cha NEC kimewataka wanachama hao kujirekebisha na kutorudia makosa yao ama sivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa katiba, Kanuni na taratibu za Chama ikiwamo kufukuzwa uanachama", imeandika Taarifa hiyo. Inaendelea/ BOFYA HAPA Usome Taarifa Kamili
Your Ad Spot
Dec 13, 2019
Home
featured
siasa
CCM YAAMURU KINA KINANA, MAKAMBA NA MEMBE WAITWE NA KAMATI YA USALAMA NA MAADILI YA CHAMA KUJIELEZA KUHUSU KUKIUKA MAADILI
CCM YAAMURU KINA KINANA, MAKAMBA NA MEMBE WAITWE NA KAMATI YA USALAMA NA MAADILI YA CHAMA KUJIELEZA KUHUSU KUKIUKA MAADILI
Tags
featured#
siasa#
Share This
About Bashir Nkoromo
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇