Waziri wa
Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Mkuu wa
Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Byakanwa mara baada ya kuwasili mkoani Mtwara
kufuatilia hali ya malipo ya wakulima wa korosho leo tarehe 13 Disemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara
Mhe Gelasius Byakanwa mara baada ya kuwasili mkoani Mtwara kufuatilia
hali ya malipo ya wakulima wa korosho leo tarehe 13 Disemba
2019. Wengine pichani ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah
Ulega na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe Evord Mmanda.
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Mtwara
Zao la
korosho katika msimu wa kilimo wa mwaka 2019/2020 limeingiza zaidi ya Bilioni
406.3 kupitia minada sita ambayo imekwishafanyika kwa nyakati tofauti.
Waziri wa
Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 13 Disemba 2019 wakati akizungumza na Mkuu wa
Mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Byakanwa mara baada ya kuwasili mkoani Mtwara
kufuatilia hali ya malipo ya wakulima wa korosho.
Waziri
Hasunga amesema kuwa kiasi hicho kimepatikana kabla ya minada itakayofanyika
kuanzia tarehe 13 Disemba 2019 na kuendelea.
Amesema
kuwa mpaka sasa tayari Tani 163,000 zimekusanywa huku Tani 151,554 zikiwa
zimeuzwa kati ya korosho hizo zilizokusanywa.
Mhe
Hasunga amesema kuwa muendelezo wa minada ya korosho inayoendelea katika maeneo
mbalimbali nchini inatoa taswira chanya kwa wakulima hivyo kuwa na uhakika wa
kipato chao kutokana na minada hiyo kuendelea kutoa matokeo chanya hususani
kuongezeka kwa bei.
Alisema
kuwa Korosho ni zao muhimu na ndilo linaongoza kwa kuiingizia nchi Pato kubwa
la kigeni likifuatiwa na zao la Tumbaku.
“Bado
hatujamaliza kukusanya korosho, hatujamaliza kuuza korosho na shunguli zingine
za serikali kusimamia zao la kilimo ikiwa inaendelea lakini mpaka sasa
tumeshakusanya zaidi ya Bilioni 406 hivyo hayo ni maendeleo mazuri kabisa”
Alikaririwa Mhe Hasunga
Ili
kuboresha zaidi sekta ya kilimo hususani zao la Korosho Waziri huyo wa Kilimo
Mhe Hasunga amesema kuwa serikali imekusudia kusimamia vyema vyama vya ushirika
ikiwa ni pamoja na kuboresha sheria yake ili kuboresha weledi wa kiutendaji kwa
wananchi.
“Tumeamua
kuchukua hatua za dhati kabisa kama serikali za kuhakikisha Ushirika
unasimamiwa ipasavyo, Ushirika unaonekana kuimarika zaidi Ruvuma, Lindi na
Mtwara kuliko maendeo ya Pamba na Kahawa. Hivyo tuna kila sababu ya kutatua
changamoto zilizopo ikiwa ni pamoja na kuboresha ushirika kote nchini” Alisema
Mhe Hasunga
Amesema
kuwa Vyama vingi vya ushirika havina uwezo wa kuweka kumbukumbu sahihi za
makusanyo, madai ya wananchi na mauzo ya korosho, baadhi ya viongozi kutokuwa
waaminifu na kuwa wabadhilifu wa mali za wananchi.
Waziri
Hasunga amesema kuwa tayari wizara ya kilimo imeanza kuchukua hatua za kisheria
kwa viongozi wote wa vyama vya ushirika ambao wamepokonya mali za wananchi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇