Afisa
Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) na Mkurugenzi
wa Kampuni ya Advent Construction Tanzania Ajith Prasad (kushoto)
wakibadilishana mkataba wa makubaliano wa uendelezwaji wa ujenzi wa
mradi wa usambazaji maji Kimbiji utakaohusisha ujenzi wa tanki la maji
lenye ujazo wa Lita milioni 15 litakalojengwa eneo la Kisarawe II na
kituo cha kusukumia maji (pumping station). Utiaji huo wa saini
umeshuhudiwa na Mbunge wa Kigamboni na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt Faustine Ndugulile, Mkuu wa Wilaya
ya Kigamboni Sarah Msafiri na viongozi wengine leo katika ofisi ya Mkuu
wa Wilaya Kigamboni.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Wakazi
wa Kigamboni wako mbioni kuondokana na kero ya upatikanaji wa maji safi
kwa muda mrefu baada ya mradi wa maji wa visima vya Kimbiji ulioibuliwa
mwaka 2005 kuanza kuendelezwa kwa kujenga miundo mbinu ya usambazaji
maji.
Mamlaka
ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA wameitia saini
mkataba wa ujenzi wa mradi wa usambazaji maji Kimbiji na kampuni ya
Advent ya Tanzania wenye thamani ya Bilioni 10.5
Mkataba
huo umetiwa saini ukishuhudiwa na Mbunge ww Kigamboni na Naibu Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Dkt Faustine
Ndugulile, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri na viongozi
wengine.
Akizungumza
kabla ya utiaji saini, Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian
Luhemeja amesema Kigamboni ni moja ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam
ambapo mtandao wa maji ni mdogo katika eneo la Navy yakitokea mtambo wa
Ruvu Chini kupitia bomba la inchi 16.
Luhemeja
amesema, mradi wa visima vya Kimbiji una visima vyenye urefu wa mita
600 na uwezo mkubwa wa uzalishaji maji na mkakati ni kuviendeleza ikiwa
na kuanza ujenzi wa miundo mbinu itakayochukua maji kutoka kwenye visima
hivyo.
Amesema,
wameingia makubaliano na kampuni ya Advent ya kujenga tanki la
kukusanyia maji kutoka visima mbalimbali (sump well) lenye ujazo wa Lita
540,000, ujenzi wa Kituo cha Kusukumia maji (pumping station), ujenzi
wa mabomba ya kusafirishia maji yenye urefu wa jumla ya km 6 hadi kwenye
tanki.
Pia, litajengwa tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa Lita Milioni 15 litakalojengwa katika eneo la Kisarawe II.
Kwa
upande wa Naibu Waziri, Ndugulile amewaongeza sana Dawasa kwa kazi
kubwa wanayoifanya ya kupeleka maji katika Mkoa mpya wa Kihuduma wa
Kigamboni kwani ni miaka mingi kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa
maji kwenye maeneo mengi ya Wilaya hiyo.
Ndugulile,
amesema mradi unachukua miezi 12 mpaka kukamilika, na utakapokamilika
utaondoa kero ya maji ya wakazi wa Kigamboni, na amefurahishwa kwa
Dawasa kuipa hadhi wilaya hiyo kuwa mkoa kamili wa kihuduma na
amewaahidi kushirikiana nao katika kuleta maendeleo.
"Nikiangalia
takwimu ya miaka ya mitatu ya nyuma, huduma ya maji kwa sasa imekuwa
san nawapongeza mnafanya jitihada kubwa za kuhakikisha maji yanapatikana
tena mnajenga miradi kwa fedha za ndani na hii ndiyo kasi anayoenda
nayo Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli
kuelekea uchumi wa kati wa Viwanda," amesema.
Makamu
Mwenyekiti wa Bodi Dawasa Laston Msongole amesema wanaendelea na
jitihada za kuhakikisha Mkoa wa Dar es Salaam unamaliza tatizo la maji
kwa kuwafikia wananchi wote hususani maeneo ya nje ya mji ambapo mtandao
wa Dawasa haujafika.
Kwa
sasa wananchi wa Kigamboni wanapata maji kutoka kwenye visima virefu
vipatavyo 29, ambapo kwa sheria mpya vinasimamiwa na Dawasa vyenye uwezo
wa kujaza Lita 225,556 kwa saa vikiwa na vizimba 151 na wateja 2,324 .
Visima
hivyo ni pamoja na Minondo, Mwasonga, Kisarawe II, Vijibweni, Geza
ulol, Ungindoni, Maweni, Puna na baadhj mengine ya maeneo.
Mradi wa maji wa Kimbiji unakuwa moja ya chanzo kikubwa cha maji chenye uhakika kwa jiji na maendeleo ya Mkoa wa Dar es Salaam.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) na Mkurugenzi
wa Kampuni ya Advent Construction Ajith Prasad (kushoto) wakitia saini
mkataba wa makubaliano wa uendelezwaji wa ujenzi wa mradi wa usambazaji
maji Kimbiji utakaohusisha ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa Lita
milioni 15 litakalojengwa eneo la Kisarawe II na kituo cha kusukumia
maji (pumping station). Utiaji huo wa saini umeshuhudiwa na Mbunge wa
Kigamboni na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na
Watoto Dkt Faustine Ndugulile, Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Sarah Msafiri
na viongozi wengine leo katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kigamboni.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mhandisi
Cyprian Luhemeja akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa
makubaliano wa uendelezwaji wa ujenzi wa mradi wa usambazaji maji
Kimbiji utakaohusisha ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa Lita
milioni 15 litakalojengwa eneo la Kisarawe II na kituo cha kusukumia
maji (pumping station) leo katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kigamboni.
Makamu
Mwenyekiti wa Bodi Dawasa Laston Msongole akizungumzia utiaji saini wa
mkataba wa uendelezwaji wa Visima vya Kimbiji kwa kujenga miundo mbinu
ya usambazaji maji, mkataba huo umetiwa saini leo katika ofisi ya Mkuu
wa Wilaya Kigamboni.
Mbunge
wa Kigamboni na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee
na Watoto Dkt Faustine Ndugulile, akiwapongeza DAWASA kwa kazi kubwa ya
kupelekamaji katika Mkoa mpya wa Kihuduma wa Kigamboni kwani ni miaka
mingi kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa maji kwenye maeneo mengi
ya Wilaya hiyo.
Mkuu
wa Wilaya ya Kigamboni Sara Msafiri akiwashukuru DAWASA kwa kufanikisha
mradi mkubwa wa maji wenye thamani ga Bilion 10.5 kuanza kutekelezwa
ndani ya Wilaya yake.
Watendaji na viongozi mbalimbali wakifuatilia hafla ya utiaji saini.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇