Meza
kuu ikiongozwa na Waziri wa Afya jinsia Wanawake na Watoto Mh, Ummy
Mwalimu , Naibu Waziri Ofisi ya Maakamu wa Rais- Mh. Mussa Sima pamoja
na Viongozi wengine waliohudhuria katikahafla ya maadhimisho ya wiki ya
usafi wa mazingira na Mkutano wa Maafisa Afya wa Mikoa wakiimbakwa
pamoja wimbo maalum wa Wafanyakazi, mkutano huo uliaandaliwa na Wizara
ya Afya jijiniDodoma.
Sehemu ya Wadau kutoka sehemu mbalimbali walioshiriki katika sherehe za maadhimisho ya wiki yausafi wa mazingira na Mkutano wa Maafisa Afya wa Mikoa, Halmashauri na Wadau ulioandaliwa naWizara ya Afya na kufanyika katika ukumbi wa Landmark jijini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Maakamu wa Rais- Mh. Mussa Sima akiongea wakati wa maadhimisho ya wiki ya usafi wa mazingira na Mkutano wa Maafisa Afya wa Mikoa, Halmashauri na Wadau ulioandaliwa na Wizara ya Afya na kufanyika katika ukumbi wa Landmark jijini Dodoma. Mgeni Rasmi katika Mkutano huo alikua Waziri wa Afya jinsia Wanawake na Watoto Mh, Ummy Mwalimu.
***************************************
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima amezitaka Halmashauri zote nchini kugawa tozo na faini zote zinazopatikana kwenye
mapato ya ndani kuzigawa kulingana na Mpango kazi wa Maafisa Mazingira waliopo kwenye Halmashauri husika.
Alisema hayo wakati alipohudhuria katika maadhimishoya wiki ya usafi wa mazingira na Mkutano wa Maafisa Afya wa Mikoa, Halmashauri na Wadau ulioandaliwa na Wizara ya Afya na kufanyika katika ukumbi wa Landmark jijiniDodoma.
“Mgawanyo lazima uende kwenye usafi na mazingira na mgawanyo ambao hauendi kwenye usafi na mazingira sisi tutambea na kusimamia hili “ alisema Naibu WaziriSima. Aliongeza kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais ndiyo yenye jukumu la kulinda, kusimamia na kuhifadhi mazingira na kusisitiza kuwa wapo Maafisa mazingira kuanzia ngazi ya Kijiji na kusisitiza kuhuisha Kamati za Mazingira.
Hivyo amewataka Maafisa Afya kuwa na ushirikiano na Kamati za Mazingira zilizopo kwenye ngazi za chini za Serikali za Vijiji, Kata na Wataalamu wa Mazingira waliopo katika Mikoa na Wilaya.
Akiongea katika warsha hiyo Mh Ummy Mwalimu alisema ni muhimu kuhamasisha vijana kuweza kujenga vyoo bora katika kila kaya kwa ajili ya kuweza kulinda afya nakuepuka magonjwa mbalimbali na kulinda mazingira. Amewataka na Halmashauri zote nchini kutimiza wajibu wa kujenga vyoo na kutolea mfano wa Wilaya ya Njombe ambao wamepiga hatua kubwa katika ujenzi wa vyoo bora kwa kila kaya na kuweza kufikia asilimia 96.
“Taarifa ya world bank inaonyesha watu wanapoteza saa 58 kwa mwaka sababu ya kutokua na vyoo . Hivyo basi Wananchi wanatakiwa kufikiria kupoteza hizo saa 58 badala ya kufanya shughuli za kuweza kujiingizia kipato na kuinua uchumu wa Nchi yetu” alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy ameunga mkono mapendekezo ya Naibu Waziri Sima katika suala la ushirikiano kati ya Maafisa Afya na Mazingira waliopo katika Halmashauri na miji.

No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇