Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii
RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaahidi wananchi wa tarafa cha Shelui Mkoani Singida kuchangia Milioni 250 kwaajili ya kujenga Kituo cha Afya katika tarafa hicho.
RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaahidi wananchi wa tarafa cha Shelui Mkoani Singida kuchangia Milioni 250 kwaajili ya kujenga Kituo cha Afya katika tarafa hicho.
Ameyasema hayo baada ya mwananchi wa Maeneo ya Shelui, Aidani Shabani kutoa kero ya kutokukamilika kwa kituo cha Afya cha Shelui kutokukamilika kwa miaka 15 sasa, kilichopo Mkoani Singida
"Lakini hapa kwetu shelui tunatatizo moja Mheshimiwa Rais, Tatizo Kubwa tulilonalo la kituo cha Afya kwenye Tarafa yatu ya Shalui, Hatuna Kituo cha Afya, kituo cha Afya tulichonacho kimeanza kujengwa sasahivi ni miaka 15, na wananchi tulichangia, alikuja kipindi anamalizia Mheshimiwa Rais Jakaya akaja akasimama pale, Akasema "Mimi kama Rais wenu Yuko wapi mwenyekiti? " Akaja mwenyekiti akasema; "Nakupongeza Sana Mwenyekiti" na Kile kituo cha Afya nitachangia akasema atachangia milioni 200 ",". Amesema shabani.
Hata hivyo Shabani amesema kuwa tangu tumeanza harakati ni miaka 15 kile kituo cha afya kipo vilevile kwani kila ajali zikitokea watu wanapoteza maisha kwasababu wanapelekwa katika hospitali ya wilaya Kihomboi mbali na lami, hivyo inakuwa shida kuwafikisha majeruhi.
"Tunakuomba Mheshimiwa kizingatie kile kituo cha Afya na ujue tatizo ni nini?, kama michango inatoka kwanini hakikamiliki? utusimamie baba kituo cha afya kikamilike".
Hivyo rais Dkt. Magufuli katika kumjibu mwananchi huyo alitaka kumtambua katibu tarafa , mtendaji wa kata na mkuu wa mkua kwaajili kujua ratiba ya kituo cha afya cha Shelui.
Baada ya kupata maelezo kutoka kwa viongozi hao, Rais Dkt. Magufuli, amesema kuwa akawashukuru wananchi hao kwa maendeleo ya eneo hilo.
"Ahadi hii ilitolewa na Rais mpendwa kikwete nataka kiwadhibitishie sasa, hizo milioni 200 nitazitoa na ziongezeke na (Madawa) dawa yaanze kupatikana vizuri. Nataka niwaahidi ndugu zangu msema kweli ni mpenzi wa Mungu huu ni mwezi wa ngapi?.... mwezi wa 11(Novemba),Mnipe mwenzi mmoja mwezi wa 12 (Desemba), kujiandaa kwa sababu kunasherehe nyingi watu mnasheherekea mwaka mpya!, mwezi wa kwanza milioni mia 200 zitakuwa hapa zinaendeleza msichange tena kwaajili ya kituo cha afya.
Kwahiyo Mkuu wa Wilaya usiwachangishe wananchi wa hapa kwa sababu ya kituo cha afya, tutakijenga tukimalizie, kama ambavyo rais wa awamu ya nne alivyoahidi, aliahidi, mimi nitatekeleza kama kijana wake, ninajua ninyi ni hamuwezi kusema uwongo, si ndio ndugu zangu?".
Katika suala la Kituoa cha Afya Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa "Hili la afya la hospitali, lazima kiwe kituo kikubwa cha afya, hizo milioni 200, tena nitaongeza na mimi nichangiepo kidogo zitakuwa milioni 250".
Rais, Dk. Magufuli amesema tatizo la maeneo ya kuegesha magari anawaachia halmashauri ya wilaya, pamoja na DC na watendaji wa eneo hilo, ili waamue wanataka kujenga maegesho ya magari wapi.
Rais Dkt. Magufuli alisimama barabara kwaajili ya kuwasikiliza wananchi waliokuwa wamekusanyika alipokuwa wakielekea Kahama mkoani shinyanga.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇