Rais Magufuli amesema kitendo cha vyama vya upinzani kususia uchaguzi wa serikali za mitaa ni demokrasia huku akisisitiza kuwa maendeleo hayana chama na Watanzania wanatakiwa kutanguliza mbele maslahi ya Taifa.
Akizungumza Leo Jumatano Novemba 27, 2019 na wananchi wa Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Rais Magufuli amekipongeza Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa ushindi katika uchaguzi huo.
“Nawashukuru sana ndugu zangu wa Isaka mmemaliza chaguzi, nimeambiwa Chama Cha Mapinduzi kimepasua vizuri. Hongereni sana, maendeleo ndugu zangu hayana chama na demokrasia hata kujitoa nayo ni demokrasia, kususia uchaguzi nayo ni demokrasia,” amesema Rais Magufuli na kuongeza;
“Kwa hiyo nawapongeza kwa ushindi mkubwa mlioupata chama cha mapinduzi lakini maendeleo hayana chama ni lazima tushikamane wote kujenga taifa letu, tunachohitaji ni maendeleo, ukileta maji, wote watakunywa, uwe CCM, uwe Chadema, ukileta bandari hapa kila mmoja atafanya biashara,”
Mhe. Rais Magufuli awapongeza Watanzania kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Ni alipowasalimu wananchi wa Igunga, Nzega na Isaka akiwa safarini kutoka Dodoma. pic.twitter.com/4tJZY2MheF— Gerson Msigwa (@MsigwaGerson) November 27, 2019
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇