Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Amos Nungu
katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
kuhusiana na mkutano wa kubadilishana uzoefu wa Masuala ya Sayansi
Techinolojia na Uzoefu unaoanza leo hapa nchini kulia ni Ofisa Mtafiti wa Costech, Neema Tindamanyire na kushoto ni Meneja Sayansi Hai kutoka Costech, Hulda Gideon.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimzikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Amos Nungu.
WAGENI 250 kutoka nchi mbalimbali duniani wamewasili
hapa nchini kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa viongozi wa Baraza la
Sayansi Kanda ya Afrika kwa lengo la kubadilishana uzoefu pamoja
kujifunza kuhusu masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Amos
Nungu akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana
kuhusu mkutano huo ambao unaoanza leo.
Alisema mada inayotawala mkutano huo ni sayansi wazi na shirikishi
katika utafiti na ubunifu wa maendeleo, hivyo Costech kama mratibu wa
masuala hayo ya utafiti, teknolojia na ubunifu imepewa dhamana ya
kuandaa mkutano huo.
“Kupitia mkutano huu tutabadilishana uzoefu pamoja na kujifunza
kutoka kwa kila mmoja, pia kujenga mahusiano pale inapowezekana,”
alisema Dk. Nungu.
Dk. Nungu alisema, Tanzania ipo kwenye sera ya uchumi wa viwanda
hivyo katika mkutano huo watajifunza mambo mengi kutoka kwa wengine kwa
kuwa nchi 16 za Afrika zinashiriki pamoja na mataifa makubwa karibu kila
bara.
Katika mkutano huo, Dk. Nungu alisema Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Dk. Joyce Ndalichako atafungua.
Kwa upande wa Meneja Sayansi Hai kutoka Costech, Hulda Gideon alisema
mkutano huo utazungumzia sayansi wazi kwa maana kuwa mawazo yote
yanayotolewa yawe shirikishi, andiko pamoja na utafiti unaofanyika kuwa
wazi na mwishoni taarifa ziwe wazi kwa ajili yaw engine kuzitumia.
Alisema sayansi wazi haiangali maandiko tu ya utafiti bali hata vifaa
vinavyotumika ambavyo vinaweza kusaidia wengine ambao hawana vifaa
hivyo.
Alisema Tanzania ni mojawapo ya nchi zinazokuza sayansi nayo
imeshiriki kwenye utafiti na data katika sekta ya afya na maliasili
ambavyo kwa Tanzania inaongelewa kuwa ina viumbe hai wengi.
“Inabidi sayansi ilivyofanyika ikatumika kuwaambia watu kuwa kuna
utafiti huo umefanyika. Hata kwa upande wa dawa unakuta mimea mingi ipo
kwa nchi za Afrika ambazo ni maskini utafiti ukifanyika huku kama hakuna
uwazi, yale maandiko yatabakia nchi zilizoendelea wataingia kwenye
viwanda vyao na kuzalisha dawa halafu sisi tunasubiri kununua dawa
kutoka kwao.
“Lakini kama tukiwa ile sayansi wazi watajua kuwa dawa zile pamoja na
kuwa zimetengenezwa kwenye viwanda vya nje lakini zilitokea Afrika ni
rahisi kushare ile keki iliyotokana na dawa hizo,” alisema.
Alisema hiyo ndiyo maana halisi ya kuhamasisha Tanzania kuingia
kwenye michakato yote ya kuwa na sayansi hai inayokuwa na uwazi zaidi.
“Lengo kubwa la kuwa na sayansi hai ni kukuza sayansi yenyewe, kama
Afrika au nchi zinazoendelea hatujafika kule lakini tukiifanya ile
sayansi ikawa wazi ina maana wale wenzetu kule nje wanachokifanya na
sisi tutakijua, tukikijua hatuna haja ya kuanza kitu upya tutatumia vile
ambavyo wamevifanya na kuvileta huku kwetu kwa ajili ya kuviendeleza,”
alisema.
Sayansi wazi pia inasaidia kupunguza gharama hivyo mtu anayefanya
utafiti wa aina hiyo nchini hatakuwa na haja ya kununua kifaa
kinachohitajika ikiwa ni pamoja na kukuza ushirikiano baada ya kujua
mwingine ana nini au anafanya nini.
Hata hivyo Ofisa Mtafiti wa Costech, Neema Tindamanyire alisema hadi
kufikia jana nusu ya wageni walioalikwa walikuwa wameshafika.
Katika mkutano huo takribani sh. milioni 500 zitatumiwa na wageni hao
kama gharama za kwenye hoteli, vyakula na huduma mbalimbali
watakazozipata nchini ikiwa ni pamoja na kutembelea vivutio mbalimbali
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇