Picha
mbalimbali za Awamu ya Pili ya muendelezo wa mradi wa kuzuia ujangili
katika vijiji vilivyopo kando kando ya hifadhi za Taifa nchini
Tanzania.
Mradi huu umefadhiliwa na Ubalozi wa China nchini Tanzania na kuratibiwa na Taasisi ya Sukos Kova Foundation.
Awamu
ya Pili ya mradi huu umehusisha msaada kwa wakazi wa kijiji cha Mhenda
wilayani Kilosa mkoani Morogoro, kijiji kilichopo kando kando ya Hifadhi
ya Taifa ya Mikumi. Baadhi ya wanakijiji wa Mhenda hasa vijana
hujihusisha na Ujangili kama njia ya kujiingizia kipato.
Ubalozi wa China nchini Tanzania pamoja na Sukos Kova Foundation umewasilisha msaada wa:
a) Mbegu za Mahindi - 2,500kgs
b) Mbegu za Alizeti - 1,500kgs
c) Mbegu za korosho- 800kgs
Msaada
huu unalenga kuwasaidia wanakijiji wa mhenda wapatao 3,000
kujishughulisha na kilimo badala ya ujangili kama njia ya kujiingizia
kipato.
Aidha misaada mingine iliyotolewa ni:
d) Uniform - 13
e) Boots - 13
Kama
njia ya kuunga mkono juhudi za kikundi cha ulinzi shirikishi wilayani
kisaki ambao ni wananchi wanaoshiriki kulinda hifadhi ya Taifa ya
Mikumi.
Pia
Ubalozi wa China na Sukos Kova Foundation wamekabidhi Kompyuta pakata
(Laptop) 4 pamoja na runinga 1 (TV set) kwa ajili ya kusaidia maafisa wa
mikumi kuelimisha zaidi wakazi wa vijiji vilivyopo kando kando ya
hifadhi hiyo kupinga ujangili na kuungana na Serikali katika kulinda na
kutunza hifadhi hizo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇