Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ameahidi kutoa
shilingi milioni 31 kwa shule ya Sekondari Misungwi ili kukamisha
ujenzi wa bweni la wasichana.
Waziri
Ndalichako ametoa ahadi hiyo mwishoni mwa wiki alioofika shuleni hapo
kukagua miundombinu ya shule hiyo ambapo amesema amefurahishwa kuona
uongozi wa shule jiyo umekuwa ukitumia fedha visiting na kuweka akiba
ya fedha kidogokidogo ambazo zimewawezesha kuanza ujenzi wa bweni hilo
"Nimefurahishwa
na mpango wa shule wa kuhifadhi fedha kidogo kidogo mpaka wamepata
fedha kwa ajili ya ujenzi wa bweni la watoto wa kike jitihada hizi ni
kazima ziungwe mkono nami nikiwa waziri wa elimu natoa mchango wangu wa
kuhakikisha naleta fedha za kumalizia " Amesema Waziri ndalichako.
Profesa
Ndalichako amesema pamoja na kutoa fedha kwa ajili ya kumalizia ujenzi
pia atahakikisha samani za bweni zinanuliwa ili bweni hilo likamilike
na kutumika.Aidha, Waziri Ndalichako amewata wanafunxi wa
kike katika shule hiyo kuzingatia masomo yao wawapo shikeni hapo na
kutojiingiza katika mambo ambayo yatawakatisha masomo yao na mwisho
kupoteza ndoto zao.
Mkuu
wa Shule ya sekondari Misungwi Mwanani Asembandwa amemshukuru Waziri wa
Elimu kwa kutambua jitihada za shule za kuweka fedha kidogokidogo kwa
ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana
Asembandwa
amesema shule hiyo imefanikiwa kuwekeza fedha kidogo kidogo mpaka
ikafanikiwa kupata miliini 44 ambazo zimetumiwa kuanza ujenzi wa bweni
la wasichana ambalo likikamilika itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi
80 kwa wakati mmoja.
"Kukamilika
kwa bweni hili kutasaidia kutatua changamoto ya sehemu ya kulala kwa
wanafunzi wa kike wa shule pamoja na kuongeza wigo wa kutoa elimu kwa
watoto wa kike wengi zaidi" Amesema Mkuu huyo wa Shule.
Naye
Mwanafunzi wa shule hiyo Zemda Robert amemshukuru Waziri kwa kutoa ahadi
hiyo ambayo inakwenda kupunguza changamoto ya malizi shukeni hapo.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akikagua eneo
linalojengwa bweni la wasichana katika shule ya sekondari ya Misungwi
Moja ya jengo la bweni la wasichana katika shule ya sekondari Misungwi lililojengwa na serikali kupitia mradi wa EP4R.
Waziri
wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na
wanafunzi wa Shule ya Sekondari Misungwi alipofika shuleni hapo
kukagua mindombinu ya shule hiyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇